ILEJE YAWANOA WAFANYABIASHARA MFUMO MPYA WA TAUSI





Wafanyabiashara wilayani Ileje mkoani Songwe watakiwa kutumia mfumo mpya wa TAUSI kulipia mapato Ili kuondoa ufujaji na upotevu wa fedha.


Wito huo umetolewa Machi 29,2023 na mkuu wa wilaya hiyo Mhe. Farida Mgomi wakati akizungumza na wafanyabiashara hao katika kikao Cha Baraza la biashara la Wilaya ambacho pamoja na agenda zingine, kulikuwa na lengo la kutoa elimu kwa wafanyabishara juu ya matumizi ya Mfumo mpya wa TAUSI.

Mgomi amesema mfumo huo ni rafiki kama alivyo ndege Tausi ambapo kwa namna moja au nyingine utaweza kusaidia  kutatua chanagamoto za  ukusanyaji wa mapato sambamba na kupunguza hoja za Mkaguzi wa nje wa Hesabu za Serikali.


Hata hivyo Mgomi ameitaka halmashauri kuwa tayari kuacha kutumia mfumo ule wa zamani wa LGRCIS na kuingia kwenye mfumo mpya wa TAUSI


"Hakikisheni mnasajili pos zote kwenye mfumo mpya wa Tausi  na makusanyo ya fedha zote zinapelekwe benki", amesema Mgomi.


Mgomi amesema serikali imekuwa ikiboresha mazingira rafiki kwa wafanyabiashara hivyo ujio wa mfumo mpya wa ulipaji Kodi imejiridhisha kwamba una tija Kwa wafanyabiashara.

Mgomi amesema kitengo Cha biashara Cha Halmashauri hiyo kijikite kutoa elimu Kila kata kwa wafanyabiashara Kwa lengo la kuwafanya wauelewe mfumo huo ambao umeletwa Kwa lengo la kuondoa usumbufu Kwa mtu au kikundi kinachotaka kuanzisha biashara.


"Elimu iendeleee kutolewa kwani wilaya ya Ileje ni kubwa na Kila siku inakua na watu kuanzisha biashara ni muhimu kueneza elimu hiyo kwa lengo la kuondoa ufujaji wa mapato sambamba na serikali ipate mapato ya kutosha Kwa maslahi ya Taifa", amesema Mgomi.


Akitoa neno la shukrani kwa niaba ya washiriki wa mafunzo hayo Mfanyabiashara Mohamed Meals amesema wanaishukuru serikali kwa kupata mafunzo hayo kwa maana ya kujifunza mfumo mpya wa ukusanyaji mapato TAUSI ambapo amesema mfumo huo utasaidia kupunguza changamoto walizo kuwa wakizipata katika mfumo ule wa awali na kwenda kufanya kazi na kuutumia mfumo huo kwenye biashara zao.


Mwala amesema wataendelea kuutumia mfumo huo na kushauri kitengo cha biashara wilaya kuhakikisha wanatoa elimu Kwa Kila mfanyabiashara ili mfumo huo ulete tija Wilayani Ileje.

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE