BILIONI 70 KUTOA MAJI MTO MOMBA HADI TUNDUMA, VWAWA NA MLOWO.



Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Dkt. Francis Michael amesema Bilioni 70 zitaanza kutekeleza mradi kwa hatua ya awali kutoa maji kutoka mto Momba na kuleta katika mji wa Tunduma, Vwawa na Mlowo kwa muda wa miezi 24, ni mradi mkubwa kwa Songwe ambao utakwenda kumtua mama ndoo kichwani.


Mkuu wa Mkoa amesema hayo baada ya kukutana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Nadhifa Kemikimba ambaye amefanya ziara Songwe kutekeleza agizo la Waziri wa Maji, Mhe. Juma Aweso alilotoa mapema wiki alipokuwa Songwe kwenye ziara ya kikazi.


Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Dkt. Francis Michael amesema kuna tatizo la upatikanaji maji katika mji wa Tunduma, Mlowo na Vwawa ambapo ni 48% tu ndio maji yanapatikana mjini wakati vijijini upatikanaji ni 78% ndio sababu ilimfanya Waziri wa Maji amuagize Katibu Mkuu aje Songwe kutoa suluhu ya mto upi utumike, tunashukuru amefika na ametupa Habari njema kuwa mradi wa kutoa maji Momba utaanza kwa Bilioni 70.


Tunamshukuru Katibu Mkuu ameunda timu ya watalamu mbalimbali kutoka sehemu mbalimbali za Nchi, wapo watalamu kutoka Tanga, Morogoro, Mbeya na kutoka Bonde la Ziwa Rukwa ambayo itaanza kazi haraka ya kuona jinsi ya kutoa maji mto Momba, Mhe. Dkt. Francis Michael.


Katibu Mkuu, Mhandisi Nadhifa Kemikimba amesema wameamua kutumia mto Momba kwa sababu kwenye sanifu za awali ilikuwa watumie mto Bupigu wa Ileje lakini baada kukusanya takwimu mto Bupigu kiangazi maji yake yanapungua tukaona sio sahihi kuweka mradi wa chanzo cha maji wa kubeba Lita milioni 70 alafu maji kiangazi maji yanapungua tukaona sio sahihi.


Lakini mto Momba una maji ya kutosha ata tukichukua lita milioni 70 bado maji yataendelea kutililika na ndio chanzo sahihi kuhudumia mji wa Tunduma ambao imekuwa na changamoto kubwa ya Maji kwa muda mrefu, amesisitiza Mhandisi Nadhifa Kemikimba


Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE