FAMILIA YA ASKARI YATEKETEA KWA MOTO

 




Baadhi ya wananchi wa mtaa wa Kaloleni Kiteto wakiwa nyumbani kwa Askari Polisi Oscar Joash aliyepoteza familia yake ya mama na mtoto kwa kuungua moto wakiwa wamelala ndani ya nyumba  usiku wa kuamkia 

Muktasari:

Ilikuwa ni hitilafu ya umeme, balbu kudondoka kitandani na kuunguza chandarua na godoro na kusababisa vifo vya familia ya mama na mtoto.

Kiteto. Ilikuwa ni hitilafu ya umeme, balbu kudondoka kitandani na kuunguza chandarua na godoro na kuabanisha vifo vya familia ya Askari Polisi Kiteto ya mama na mtoto.



Akizungumza na Mwananchi Digital Kamanda wa Jeshi Jesho la Polisi Manyara RPC, George Katabazi leo Aprili 21, 2023 amewataja marehemu hao kuwa ni Nurya Mkondya (18) na mtoto wake Joas Oscar miaka (2) wa familia ya Askari Polisi Kiteto.


"Uchunguzi wa awali unaonyesha kwamba ilikuwa ni hitilafu ya umeme yaani balbu ilidondokea kitandani na kuunguza chandarua pamoja na godoro hali iliyopelekea vifo vya mama na mtoto wakati wamelala usiku wa saa tisa kuamkia leo," amesema

Niwashukuru majirani na wananchi kwa ujumla ambao kwa namna ya pekee walivyoweza kujaribu kunusuru maisha ya familia hiyo, mama na mtoto wake lakini baada ya kuzidiwa na moshi nakukosa hewa chumbani walipoteza maisha.


"Kwa kweli walijitahidi sana kuokoa uhai wao lakini  ilishindikana," amesema RPC Katabazi.


“Wananchi walivunja mlango lakini bahati mbaya hawakufanikiwa kuokoa mama na mtoto huyo kwa kukosa hewa na kuungua sehemu mbalimbali za miili yao,” amesema RPC Katabazi.


Kamanda Katabazi ametoa pole kwa familia hiyo na askari wa kata zote (wakaguzi) wa vituo kwa tukio hilo akisema ni la kusikitisha sana kwa askari huyo kupoteza familia yake.


"Hii ni familia ya askari sisi tunaishi kama familia moja ndugu moja mwenzetu anapopatwa na janga ni pigo kwetu sote hasa kupoteza mtoto na mama yake kwa wakati mmoja inasikitisha. Kwa hiyo niwape pole familia  ya askari mwenzetu Oscar Joash kwa sasa aendelee kuwa na utulivu pamoja na subira tumwombee kwa Mungu katika kipindi hiki kigumu," amesema.


Kwa upande wa majirani walieleza kuwa haikuwa rahisi kuokoa familia hiyo kwa kuwa moshi wa kuungua godoro ulitanda chumba kizima hiyo walipoteza maisha kwa kukosa hewa kisha kuungua sehemu mbalimbali za miili yao.


"Tulifika usiku wa saa tisa baada ya watu kuomba msaada na kuvunja mlango kisha kuingia ndani haikuwa rahisi kuingia, lakini mwishowe hatufanikiwa kumwokoa mama wala mtoto wake walikuwa ndani wamelala," amesema Shabani Sendalo Mwenyekiti wa Mtaa wa Kaloleni.

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE