MBOZI YAPATA MGAWO WA SHILINGI 1.7 BILIONI UJENZI WA MIUNDOMBINU ELIMU YA AWALI, MSINGI
MBOZI. Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe imepata Shilingi Bilioni 1.7 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya elimu ya awali na msingi katika shule 10.
Fedha hizo ni kati ya Shilingi Bilioni 7.1 ambazo zimetolewa katika Mkoa wa Songwe kutekeleza mradi wa BOOST kwa mwaka wa fedha 2022/2023.
Fedha hizo zimetolewa kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya vyumba vya madarasa, matundu ya vyoo, madarasa ya wanafunzi wenye mahitaji maalumu na madarasa ya elimu ya awali ya mfano.
Shule ambazo zitanufaika na mradi huo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi ni pamoja na Lutumbi, Namlonga, Itete, Mlowo na Mabatini.
Shule zingine ambazo zitanufaika na mradi huo ni Tazara, Mlangali, Idunda, Nuru na Isangu.
Comments