MWALIMU ADAIWA KUBAKA MKOANI SONGWE
Wakati jamii ikitegemea walimu kuwa sehemu ya malezi kwa watoto hali hiyo imekuwa tofauti kwa mwalimu Tunu Brown(37)wa shule ya msingi Senjele kutoroka kituo cha kazi baada ya kutuhumiwa kumbaka mwanafunzi wake wa darasa la sita.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe Theopista Malya amethibitisha kutokea kwa Tukio Hilo Lililotokea Aprili 17 Mwaka Huu Majira Ya Saa 4:45 Asubuhi alibakwa na mwalimu wake ambapo alimlaghai mtoto kuwa atakuwa akimsaidia shida zake ambalimbali alizonazo nyumbani kwao Lakini Mwalimu Huyo Ametoroka Hivyo Jeshi La Polsi Linaendelea Na Jitihada za Kumtafuta.
Aidha Malya ametoa wito kwa jamii kuacha kufumbia macho vitendo vya ukatili dhidi ya watoto.
Naye Rose Mwampashi Bibi wa mwanafunzi amesema amewalea watoto katika mazingira magumu Huku Babu Wa Mwanafunzi Huyo Akiomba Serikali Iweze Kumsaidia Kumkamata muhusika Wa Tukio hilo la ukatili.
Kwa Upande Wake Thabitha Bugali Mkurugenzi wa Sauti ya Mama Africa mbali ya kusikitishwa na tukio hilo ameomba sheria ichukue mkondo wake
Comments