RC SONGWE AITAKA JAMII KUPUUZA UZUSHI JUU YA CHANJO ZA WATOTO


 Na Baraka Messa, Songwe

MKUU wa mkoa wa Songwe Dkt Francis Michael ametoa rai kwa jamii Mkoani Songwe kuepuka taarifa za upotoshaji kuhusu huduma za chanjo zinazotolewa nchini kuwakinga watoto chini ya miaka mitano wasishambuliwe na magonjwa mbalimbali ambayo husababisha vifo.


Alisema chanjo zinazoendelelea kutolewa Nchini na Duniani kwa Ujumla ni kwa ajili ya kupunguza vifo vinavyozuilika vitokanavyosababishwa kutokana na kukosa Kinga muhimu mwilini.


Mkuu wa mkoa Dkt Francis alisema hayo jana katika uzinduzi wa wiki ya chanjo kwa watoto wadogo chini ya miaka mitano , ambapo kimkoa imezinduliwa katika Kata ya Isongole Wilaya ya Ileje .


" Hizi chanjo ni salama zinatusaidia sana tusidharau, watalaam wanasema usipo ziba ufa utajenga ukuta tusijenge ukuta kwa kupoteza maisha ya watoto wetu, tuwakinge watoto wetu tusipotoshwe na manenonya watu ya kufananisha chanjo hizi na Mila potofu zinazotolewa na baadhi ya watu wachache" alisema Mkuu wa Mkoa.


Alisema miaka ya huko nyuma watoto wengi walipoteza maisha kutokana na kukosa chanjo hizi muhimu .alitaka Jamii kupeleka watoto kwa wingi katika vituo vya afya na zahanati zilizopo karibu na maeneo yao.


"Sisi tumefikia hatua hii na kuwa viongozi ni kutokana na kupata chanjo za polio, Pepo punda na  chanjo zingine, wazazi ,walezi ,walimu na viongozi toeni elimu kwa watoto wa shule kuhusu umuhimu wa Chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi kwa watoto wenye kuanzia miaka 14" aliongeza Mkuu wa Mkoa Dkt Francis


Naye Mganga Mkuu wa mkoa wa Songwe Dkt Boniface Kasululu akielezea Hali ya chanjo mkoani Songwe alisema mwaka 2022 mkoa ulifanikiwa kufikia lengo na kuvuka lengo la kitaifa ambalo ni kufikia asilimia 90. 


Alisema mkoa ulifikia na kuvuka malengo kwa kufiki asilimia 103 baada ya kuwafikia watoto 49885 wakati malengo ya mkoa awali  ilikuwa  kuwafikia watoto 48306 wenye umri chini ya miaka mitano  .


Dkt Kasululu alisema pamoja na mafanikio hayo Kuna baadhi ya chanjo hazikufanikiwa kufikia kiwango Cha asilimia 90 , anazitaja kuwa ni pamoja na chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi inayo tolewa kwa watoto wa kike wenye kuanzia miaka 14 na chanjo ya magonjwa ya kuhara kwa watoto chini ya mwaka mmoja.


"Kwa upande wa Chanjo ya Saratani ya mlango wa kizazi awamu ya kwanza uchanjaji dozi ya kwanza ulikuwa asilimia 63 na dozi ya pili ilikuwa asilimia 52.lakini magonjwa ya kuhara kwa watoto chini ya  mwaka mmoja dozi ya kwanza ilitolewa kwa asilimia 79 dozi ya pili ilitolewa kwa asilimia 73" alisema Dkt Kasululu.


Kwa upande wake Rehema Mbughi alisema watalaam wamekuwa wakijitahidi kutoa elimu ambayo imewasaidia wao kufuatilia dozi zote za chanjo kwa watoto chini ya miaka mitano.


Alisema changamoto inajitokeza kwa baadhi ya vijiji ambavyo vipo mbali na having zahanati wala vituo vya afya watalaam hushindwa kuvifikia wakati wa Chanjo.


Neema Kibona alisema mkazi wa Kijiji Cha Izuba wilayani humo alisema kwa wale waoishi vijijini bado Kuna changamoto ya kufikiwa na chanjo kutokana na uchache wa watalaam wa afya

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE