SIMBA YATOLEWA KWA MATUTA KIUME
Simba SC imetolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mikwaju ya penalti 4-3 baada ya kumaliza dakika 90 kwa usawa wa mabao 1-1 katika mechi mbili za robo fainali dhidi ya Wydad.
Mechi hiyo iliyopigwa kwenye Uwanja wa Mohammed V jijini Casablanca nchini Morocco, Simba haikuwa na mabadiliko katika kikosi chake kilichoanza mechi ya Dar na iliruhusu bao dakika ya 24 likifungwa na Bouly Sambou kwa kichwa lililosalia hadi dakika 90 (1-0).
Simba iliziba njia za Wydad kwa muda mwingi licha ya makosa machache waliyofanya ambayo wapinzani hawakutumia vizuri.
Wydad ambaye ni bingwa mtetezi wa Ligi ya Mabingwa alifanya mabadiliko ya wachezaji wanne ambao waliingia kwa awamu mbili huku Simba wakifanya mabadiliko ya wachezaji wawili Erasto Nyoni aliyechukua nafasi ya Jean Baleke na Kibu Denis nafasi yake alichukua Moses Phiri dakika za nyongeza.
Katika penalti tano Simba waliofunga ni Erasto Nyoni, Saido Ntibazonkiza na Moses Phiri huku waliopoteza ni Shomari Kapombe na Clatous Chama.
Wydad ambaye ametangulia nusu fainali anasubiri mshindi wa mechi ya Mamelodi Sundowns dhidi ya CR Belouizdad itakayopigwa leo Aprili 29.
Comments