WAFANYABIASHARA 13 WAFARIKI DUNIA RUVUMA

 


Wafanyabiashara 13 wamefariki dunia na wengine wawili kujeruhiwa usiku wa kuamkia leo, April 10, 2023, baada ya gari walilokuwa wakisafiria kutoka mnadani, Mitsubishi Fuso lenye namba za usajili T800 BXB, kutumbukia mtoni mkoani Ruvuma.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Marco Chilya amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa gari hilo limetumbukia katika Mto Njoka wakati wafanyabiashara hao wakitoka wakitoka Ndongosi mnadani kuelekea Kijiji cha Namatuhi wilayani Songea.

Amesema kuwa gari hilo lililokuwa likiendeshwa na Thobias Njovu, lilipofika kwenye eneo la daraja hilo, wakati linapanda mlima ghafla liliacha njia na kutumbukia mtoni.

Kamanda Chilya amesema kuwa maiti zimehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Serikali ya Mkoa wa Songea.

Aidha Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma linaendelea kusisitiza wananchi kuacha kupanda magari ya mizigo wanapokuwa wanakwenda kwenye minada na polisi hawatasita kuchukua hatua kali dhidi ya yeyote atakayekiuka agizo hilo.

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE