WAISLAMU SONGWE WAWAJIA JUU WABUNGE WA MKOA WA SONGWE JUU MBELE YA RC WADAI USHIRIKIANO KWAO ZIRO
Waislamu Mkoani Songwe wamewajia juu Wabunge wa Mkoani Songwe kwa kile walichodai kuitenga dini ya kiislamu na pindi wanapokaribishwa katika shughuli zozote za dini hiyo hawajitokezi wala kuchangia chochote lakini pia hawadhulii shughuli zozote za kimaendeleo haya yakiwa ni Malalamiko ya pili dhidi ya Wabunge hao ambapo Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Songwe pia aliwahi kuwalalamikia Wabunge hao pia kutokuwa na ushirikiano na chama chao
Akiongoa katika futari ilioandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe Sheikh wa Mkoa wa Songwe Huseein Issa Batuza amesema katika kipindi cha miaka 10 wamefanya kila jitihada za kuwaalika Wabunge wa Mkoa wa Songwe mpaka kufikia hatua ya kuwajulisha Viongozi wa CCM lakini bado baadhi ya Wabunge hao wamekuwa wagumu kuitikia wito.
"Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa Waislamu tunafanya shughuli za Maendeleo kuunga juhudi za Rais wetu na kauli ya kazi iendelee tuna ujenzi wa Zahanati, Vituo vya afya tukiwaalika hawafiki hata katika Vitabu vya Mungu vinasema ishi na Watu Vizuri havijasema ishi na Waislamu Vizuri bali na watu na Nchi yetu imejengwa katika misingi ya mapenzi na mahusiano mema ya dini zote tunaishi pamoja haya nawakumbusha Wabunge wa Mkoa huu"-Ameyasema Sheikh Batuza
Kwa Upande wake Mkuu Mkoa wa Songwe Dkt Fransis Michael amewataka Waumini wa Kiislamu kuishi kwa kupendana na kuendelea kutoa mafundisho ya kuhimiza Amani na kukemea vitendo viovu katika jamii
Katika Iftah hiyo ilioandaliwa na Mkuu wa Mkoa ilihudhuliwa na Viongozi mbalimbali wa dini na Serikari akiwemo katibu Tawala Mkoa wa Songwe Happynes Seneda Wakuu wa Wilaya akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Ileje Farida Mgomi na Viongozi wengine mbalimbali ngazi ya Wilaya na Mkoa
Comments