ILEJE WAKUTANA KWENYE FUTARI YA MKUU WA WILAYA... USHOGA WAKEMEWA
Mkuu wa wilaya ya Ileje mkoani Songwe Mhe. Farida Mgomi ameandaa Futari iliyowakutanisha waislamu, viongozi wa dini ya kikristo,viongozi wa vyama vya siasa viongozi wa Mila na viongozi wengine wa serikali.
Mhe. Mgomi ameandaa Futari hiyo iliyowakutanisha Leo Aprili 18,2023 katika Ikulu ndogo ya wilaya hiyo.
Mhe.Mgomi amewasihi waisilamu na wakristo kuwa wamoja kwa kuzingatia vitabu takatifu na kila mtu kwa nafasi yake wapendane bila kujali itikadi ya kidini.
Katika hatua nyingine Mhe. Mgomi ameungana na viongozi wengine kukemea masuala ya ushoga huku akisema serikali haitavumilia watu wanaoendekeza mapenzi ya jinsia Moja .
"Tutumie kipindi hiki Cha ramadhani kukemea vitendo viovu vinavyohatarisha utamaduni wetu ikiwa ni pamoja na kuwaripoti watu au taasisi zinazotoa elimu ya kujihusisha na mapenzi ya jinsi Moja", amesema Mgomi.
Akizungumza katika hafla hiyo shekhe wa wilaya Khamis Adamu amesema lengo la Futari hiyo ni kujumuika pamoja katika mwezi mtukufu wa Ramadhan kama ishara ya kutenda wema, kufanya ibada na kuimarisha undugu katika kuienzi dhana ya toba na upendo kwa wananchi wake.
Kwa upande wao viongozi wa dini mbalimbali walipopata fursa ya kuzungumza akiwepo Paroko Parokia ya Itumba Sililo Mwankuga Mwalyoyo amemshukuru mkuu wa wilaya kwa kuandaa ibada ya futari iliyowakutanisha pamoja katika kipindi kipindi hiki Cha ramadhani hivyo kuahidi umoja huo uendele bila kujali itikadi ya dini.
"Sisi kama Viongozi wa dini kupitia makutano haha tutumie fursa ya kuwaimba wanaileje kuliombea taifa Ili liondokane na vitendo vya jinsia Moja na kuyakemea kwa pamoja kama viongozi wa dini", amesema Mwalyoyo.
Akizungumza kwaniaba ya viongozi wa Mila Chifu Msongole amesema viongozi wa dini na Mila watumie umoja huo wa Iftari ya iliyoandaliwa na mkuu wa kujenga umoja ,upendo na mshikamano Kwa kuenzi Mila na desturi za kitanzania
Comments