WAVAMIA SHAMBA LA EKARI 4 MBOZI NA KUFANYA UHARIBIFU MKUBWA

 


Watu wasiojulikana wamevamia na kuharibu eka nne za shamba lenye kahawa, migomba na miparachichi na kuibua taharuki katika kijiji cha Haraka Kata ya Hezya wiayani Mbozi mkoani Songwe.


Tukio hilo hilo limetokea usiku wa kuamkia Ijumaa Aprili 28, 2023 wakati mmiliki wa shamba hilo, Mariam Mathias na majirani wakiwa wamelala.


Akizungumza akiwa kwenye shamba hilo,  mmoja wa wanafamilia wa mmiliki wa shamba hilo, Jane Kalupanda amesema kuwa tukio hilo limewashangaza ambapo mpaka sasa hawajafahamu waliohusika na uharibifu huo.


"Tumesikitishwa sana na kitendo hiki cha kinyama. Shamba hili ni zaidi ya eka nne ambalo kuna kahawa, miparachichi na migomba vimekatwa, tunaomba Serikali hasa Waziri wa Kilimo na Polisi watusaidie kuingilia kati ili waliofanya huu unyama wakamatwe" amesema Jene akiwa kwenye shamba hilo akionyesha mazao hayo yalivyoharibiwa.


Naye Gipson Mwayela ambaye ni ndugu wa wenye shamba  amesema tayari washatoa taarifa kwenye vyombo vya usalama akiomba Jeshi la Polisi lichunguze kubaini waliofanya uharibifu huo wachukuliwe hatua.


Kwa upande wake Mtendaji wa Kijiji hicho, Alli Irembe amesema tukio hilo limezua taharuki katika kijiji hicho.


"Baada ya kupata taarifa nilienda nikaitisha mkutano wa hazara ukiwahusisha wananchi wa vitongoji vya kijiji hicho na kijiji cha Hezya ambapo tuliuliza kama wanafahamu waliofanha tukio hilo lakini hakuna aliyesema kuwa anafahamu" amesema  mtendaji huyo wa kijiji na kuongeza;

"Kwa sasa tumeviachia vyombo vya usalama kwa ajili ya hatua za kiusalama kwa kuwa tayafi taarifa ilisharipotiwa polisi" amesema 


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Kamsishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Theopista Mallya amethibitisha kupokea taarifa hiyo na amesema tayari vyombo vya ulinzi na usalama viko kwenye eneo hilo kwaajili ya uchunguzi.


"Ni kweli taarifa hizo nimezipata na kwa sasa askari na wapelelezi wapo kwenye eneo la tukio kufanya uchunguzi ili kubaini waliofanya uharibidu huo" ameeleza


Kamanda Theopista amesema kuwa bwana shamba pia yupo kwenye eneo la tukio kufanya tathimini ya uharibifu huo.


Wakati familia ikisema ukubwa wa shamba hilo ni eka nne, kamanda Theopista amesema taarifa alizozipata ni kwamba shamba hilo lina ukubwa wa eka 2.5.

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE