WAZIRI ASHTAKIWA KWA WIZI WA MABATI



 Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Uganda ameidhinisha mashtaka ya ufisadi dhidi ya Waziri wa Masuala ya Karamoja Mary Goretti Kitutu kuhusu jukumu lake katika kashfa ya mabati eneo la kaskazini-mashariki.


Spika wa bunge na baadhi ya mawaziri pia wametajwa katika kashfa hiyo iliyohusisha madai ya wizi wa mabati 5,500 yaliyokusudiwa kwa wahanga wa maafa katika mkoa wa Karamoja.


Mwendesha mashtaka Jumatano alisema Bi Kitutu, ambaye kwa sasa anazuiliwa na polisi, Alhamisi atashtakiwa mahakamani kwa ufisadi.


Waziri wa Uganda ashtakiwa kwa kashfa ya karatasi Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Uganda ameidhinisha mashtaka ya ufisadi dhidi ya Waziri wa Masuala ya Karamoja Mary Goretti Kitutu kuhusu jukumu lake katika kashfa ya mabati katika eneo la kaskazini-mashariki.


“Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka imeidhinisha mashtaka ya rushwa na kula njama ya kutenda kosa dhidi ya Mhe. Kitutu Mary Goretti Kimono kwa kubadilisha mabati yaliyokusudiwa kwa Mpango wa Uwezeshaji Jamii ya Karamoja,” taarifa ilisema.


Polisi wameagizwa kumpeleka waziri huyo mahakamani kwa ajili ya kujibu.


Anatarajiwa kutumia likizo ya Pasaka katika gereza la Luzira ambapo atazuiliwa na Mahakama ya Kupambana na Ufisadi baada ya kushtakiwa, vyombo vya habari vya nchini vinaripoti.


Rais Yoweri Museveni ametoa wito wa kufunguliwa mashtaka kwa wale wote watakaopatikana na hatia

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE