MRADI MKUBWA WA MAJI ITELEFYA MOMBA KUMALIZA SHIDA YA MAJI WAKAZI ZAIDI YA 2,400
Mradi wa Maji unaotekelezwa na Ruwasa wenye ujazo wa lita 100,000 uliojengwa katika kijiji cha itelefya kata ya Mkulwe Wilayani Momba kwa fedha za program ya kwa matokeo (PforR) umetajwa kutekelezwa kwa asilimia 95 ambapo zaidi ya Wananchi 2,448 wanatarajiwa kunufaika na mradi huo.
Ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe kukagua miradi ya maendeleo Mkoani Songwe ilitembelea mradi huo huku Katibu tawala wa Mkoa wa Songwe Happiness Seneda akiwa pamoja na wataalamu mbalimbali waliutembelea mradi huo.
Akisomewa taaarifa ya mradi huo na Kaimu Meneja wa Ruwasa Wilaya ya Momba Injinia Beatus Katabanzi amesema mradi huo kutekelezwa 2022 na bajeti ya shilingi 445,670,000,00 na mpaka sasa mradi huo umeghalimu kiasi cha shilingi 348,757,051,91 ambapo amesema fedha hizo zimetumika katika Ujenzi wa nyumba ya pump, Vituo 8 vya kuchotea maji, ufungaji wa jenereta,ufungaji wa pump kwenye kisima pia uchimbaji wa mitaro pamoja na ulazaji wa bomba kilomita 6.3.
Akiongea mara baada ya kusomewa taarifa hiyo Seneda aliwapongeza Ruwasa kwa usimamizi wa mradi huo mkubwa na kuwataka kujikita zaidi na kuwapelea wananchi Maji majumbani kwani hapo watakuwa wametekeleza kauli ya Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ya kumtua Mama ndoo kichwani moja kwa moja badala ya kujenga vituo tu vya kuchotea maji.
Aidha katibu tawala alimtaka kaimu meneja kuzipitia jumuiya za watumia maji upya hasa suala la utoaji pesa akaunti za jumuiya hizo pia jumuiya hizo ziangaliwa kwenye suala la kuziunganisha kwani inaonyesha jumuiya hizo zimeunganishwa kata zaidi ya 3
Ziara ya Ukaguzi wa miradi Mkoani Songwe leo itaendelea katika Halmshauri ya mji wa Tunduma na itamalizika katika Halmashauri ya Songwe ambapo ziara hiyo imekwisha kagua miradi ya Wilaya za Mbozi, Ileje na Momba
Comments