MRADI WA ELIMU VIJANA CHANGAMANI (IPOSA) WAZINDULIWA ILEJE


 

Mradi wa Elimu  ya Vijana Changamani(IPOSA) wenye thamani ya Zaidi ya Shilingi milioni 85 umezinduliwa rasmi wilayani Ileje mkoani  Songwe huku matarajio ya kuwainua vijana kiuchumi ukiwa ni moja ya malengo makubwa.


Akizungumza na baadhi ya wakuu wa idara na vitengo na baadhi ya madiwani  waliohudhuria uzinduzi wa mradi huo Mei 29,2023  uliofadhiliwa na UNCEF mkuu wa wilaya ya Ileje Mhe. Farida Mgomi amesema mradi huo umekuja kwa mda mwafaka wakati dhamira ni kuhakikisha vijana wananufaika kiuchumi.


Mhe. Mgomi amesema mradi huo unatarajia kuwasaidia vijana walioshindwa kumaliza masomo au kuendelea na masomo ya sekondari na msingi kwa kuwasidia kupata elimu ya ufundi katika shule maalumu ambayo itanzishwa katka kata ya Chitete wilayani humo.


Mhe.Mgomi amesema lengo la mradi ni kuwasidia vijana kutoka mtaani,waliopata mimba za utotoni,ndoa za utotoni kupata ujuzi wa ufundi na hatimaye kuanzisha vikundi na viwanda vidogovidogo kupitia mradi huu Kwa lengo la kupunguza vijana tegemezi.


Hii ni fursa kwetu sote wanaileje ,hivyo madiwani tutumie vikao vyetu vya maendelo ya kata kuhamasisha wazazi kuwapeleka watoto wao kwenye kituo cha Chitete ili wapate fursa ya elimu hiyo kwa kujiendeleza kiufundi bila kutumia gharama yoyote”, amesema Mhe. Mgomi.


"Nikuelekeze mkurugenzi wa halmashauri ya Ileje hakikisha vikundi vya vijana vitakavyoundwa baaada ya kupata ujuzi kupitia mradi huu vinaendelezwa Kupitia idara ya maendeleo ya jamii ili wanufaike Kwa kujiingizia kipato",amesema Mhe. mgomi.


"Tuwashukuru UNICEF kwa kutuletea mradi huu wambapo kwa mkoa wa Songwe tumekuwa miongoni mwa halmashauri zitakazonufaika hivyo vifaa vitakavyonunulia visaidie kuleta tija kwa vijana”, ameendelea kueleza Mhe. Mgomi.


Sambamba na hilo Mhe. mgomi amesema vifaa vya kufundishia vitunzwe na wasimamizi kwani vimenunuliwa Kwa bei kubwa kupitia wadau wetu UNICEF ili vidumu Kwa mda mrefu Kwa manufaa ya mradi.


Kaimu mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Hermani Njeje amesema vijana watakaonufaika kupata ujuzi wa wa ufundi kupitia huu mradi itawasaidia kuinuka kiuchumi na maendeleo ya wilaya kiujumla hali itakayosaidia kuondokana na makundi yasiyofaa.


Kwa upande wake mratibu mkuu wa UNICEF Tanzania Dr.Sempeho Siafu amesema mradi huo utakuwa msaada kwa vijana kwa kuendelea kiuchumi kwa kuunda vikundi, na kuwaunganisha na wasimamizi wa viwanda vidogovidogo SIDO ili kuboresha biashara zao.

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE