TUZO ZA WANAWAKE WA MFANO ZAFANA SONGWE, RAS SENEDA AWAKUMBUSHA WAJIBU WA MWANANKE NDANI YA FAMILIA
Wanawake wa Mkowa wa Songwe wametakiwa kutambua wajibu wao katika jamii ikiwa ni pamoja na suala la maadili kwa watoto ili kuepuka vitendo vya ukatili wanavyofanyiwa watoto.
Rai hiyo imetolewa leo Jumapili Mei 14, 2023 naKatibu Tawala wa Mkoa wa Songwe (RAS), Happiness Seneda wakati akizungumza katika utoaji wa tuzo za Wanawake wa Mfano Mkoa wa Songwe 2023 zilizotolewa katika ukumbi wa Staples Chapwa wilayani Momba mkoani Songwe.
Tuzo hizo ambazo zinaandaliwa na The Great Team Event Planers zimetolewa kwa mara ya nne mfululizo ambazo zilianza kutolewa mwaka 2020 zinalenga kuwainua na kuwatambua wanawake wa mfano katika jamii ndani ya mkoa wa Songwe.
RAS Seneda amesema "Kila mwanamke ajue wajibu wake, Baba ajue wajibu wake na mama ujue wajibu waka" amesisitiza RAS
"Unatakiwa utekeleza majukumu yako kwa malezi ya watoto. Mambo ni mengi lakini hayajawahi kushinda kuangalia watoto wako" amesema
Amewataka wanawake hao kuwa karibu na watoto wao ili wajue matatizo yanayowakabili.
"Kuwa karibu na watoto wako ili kujua wamekutana na nini shuleni.Tafadhali jitahidi kutenga muda wa kuwaangalia watoto wako" amesisitiza
Amesema kuwa takwimu zinaonyesha kuwa kuna vitendo vya ukatili wanafanyiwa watoto hasa katika mji wa Tunduma hivyo wazazi wawe makini.
"Watoto wetu wanabakwa sana, watoto wetu wanalawitiwa sana nani awaokoe watoto hawa?
Hatuwatazami watoto, akina mama hali ni mbaya nawaomba tufuatilie watoto wetu" amesisitiza.
Pia amewataka wanawake hao kutokuvumilia ukatili hasa kwa wale wanaopigwa na waume zao.
Comments