UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI NAMBALA-MBOZI WAPONGEZWA

Mradi wa Ujenzi wa shule ya sekondari ya Nambala iliopo Kata Mlowo Wilayani Mbozi ambayo kwa sasa ina jumla ya wanafunzi 173 wavulana 75 na wasichana 98 ikiwa na jumla ya waalimu 9 ambayo mpaka sasa imegharimu kiasi cha shilingi
502,380,000  katika kiasi hicho Halmashauri ya Mbozi kupitia Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Abdallah Nandonde imetoa kiasi cha shilingi 29,800,000 kupitia mapato ya ndani ya halmashauri ya Mbozi.

Wiki iliopita tarehe 8 mei 2023 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa ilifanya ziara ya ukaguzi wa mradi huo ikiongozwa na Katibu Tawala Mkoa wa Songwe Happiness Seneda akiwa ameambatana na wataalamu toka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wakiongozwa na Afisa Elimu Mkoa Michael Ligola ambapo walikagua majengo ya shule hiyo ikiwepo madarasa 8,ofisi 2 za waalimu  majengo hayo yamekamilila na yanatumika aidha walikagua maabara 3 za fizikia, kemia na biolojia ambazo zipo hatua za mwisho za ukamilikaji.

Ujenzi wa matundu 20 ya vyoo, jengo la utawala, maktaba, chumba cha tehama na tenki la maji ambavyo pia vimekamilika.

Katika ziara hiyo Seneda aliwapongeza halmashauri ya Mbozi kwa usimamizi mzuri wa Ujenzi wa Shule hiyo na kuwataka kuhakikisha maeneo ambayo yamebaki katika ukamilishaji wa shule hiyo yafanyike kwa haraka ili wanafunzi waendelee kusoma pasipo vikwazo vyovyote.

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE