WANANCHI WALALAMIKIA UKOSEFU WA MAJI VWAWA LICHA SERIKALI KUJENGA MIRADI MIKUBWA



 Wananchi wa kata ya Vwawa kitongoji cha Majengo yamelalamika kutopatatikana kwa Maji katika majumba yao na sehemu za taasisi zikiwemo shule za Haloli na Nuru. Wananchi hao wakiongea mbele ya Katibu Tawala Mkoa wa Songwe wakati akikagua Ujenzi wa Mradi wa Maji unaojengwa kata ya Vwawa Wananchi hao wamesema maji mara nyingi huwa hayatoki na yakitoka ni mara moja kwa wiki. 


Wakiongea mara baada ya katibu tawala kumaliza kukagua maradi huo Wananchi wa kitongoji cha Majengo na Vitongoji vingine pia wameshangazwa na kitongoji kilichojengwa mradi huo kutosambaziwa huduma ya maji.


"Katibu tawala sisi ndio walinzi wa mradi huu mnaoukagua leo lakini sisi si wanufaika wa mradi huu tulikua tunaomba angalau mtufikirie na sisi tuweze kusambaziwa maji haya" alisema mwananchi Assani Tuja makazi wa majengo


Mwananchi Leonard Mboya mkazi wa kata ya Vwawa amedai kuwa maji yamekuwa ni changamito licha ya serikali kujitahidi kujenga miradi mikubwa ya maji kwani kata ya Vwawa maji yamekuta ni changamoto na hata yakitoka basi ni mara moja kwa wiki


Nae Rose Mwanawima makazi wa Ilembo alimueleza katibu tawala kuwa shule za Haloli na Nuru hazina maji licha ya kuwepo jirani na mradi huo.


Akijibu maswali ya wananchi hao katibu tawala aliwataka meneja wa Ruwasa Wilaya ya Mbozi na Mamlaka ya mji kuhakikisha wanayafuatilia maeneo yenye changamoto ya maji kutotoka na kuyafanyia kazi na akasema inawezekana maeneo hayo yanashida za kimiundo mbinu hivyo yafutailiwe lakini aliwataka kuangalia ni namna gani shule za Msingi za Haloli na Nuru zinaondolewa changamito ya Maji


Katibu tawala jana alifanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali katika Wilaya ya Mbozi ziara ambayo inafanya na Mkuu wa Mkoa wa Songwe pamoja na wataalamu toka ofisi ya Mkuu wa Mkoa

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE