DC AWATAKA SKAUTI KUFANYA KAZI KWA WELEDI KWANI NDIO SIRI YA MAFANIKIO YAO



Mkuu wa Wilaya ya Mbozi (DC), Esther Mahawe amewataka wahitimu wa mafunzo ya skauti wilayani humo kuweka vizuri njozi zao na kutamani kuwa watu wa viwango vya juu bila kujali hali za maisha walizotoka katika familia zao.


Pia, amewaasa kuwa kufanya kazi kwa bidii na nidhamu ni nguzo ya mafanikio katika maisha.


Mkuu huyo wa Wilaya ameeleza hayo leo Alhamisi Juni 8, 2023 wakati akifunga mafunzo ya skauti  katika wilaya hiyo.


Jumla ya vijana 119 walioweka kambi katika Shule ya Sekondari Vwawa  wamehitimu mafunzo ya skauti kutoka katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo.


Akihitimisha mafunzo hayo, DC Mahawe ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo amewaambia wahitimu hao "Hata ninyi mnaweza haijalishi background za familia zenu, iweke vizuri njozi kuwa unataka kuwa nani badaye, 


Nakuhakikishi ukimuomba Mungu, ukifanya kazi kwa bidii, ukisoma kwa bidii utaishika njozi yako ndani ya muda mfupi sana" amesema 


Amesema ili waweze kufanikiwa wanapaswa kutamani kuwa watu wa viwango vya juu.


"Tamani kuwa mtu wa viwango vya juu. Jitahidini sana na someni kwa bidii" amesisitiza 


Amewataka wahitimu wa kike kuepuka tamaa ambazo zinaweza kusababisha kuingia kwenye mahusiano ambayo yanaweza kukatisha ndoto zao za elimu.


"Watoto wa kike ninyi ni tumaini la taifa, focus kwenye njozi yako, soma kwa bidii na fikia njozi yako utakuja kuolewa huko badaye" amewasihi


Katika risala ya Chama Cha Skauti Tanzania Wilaya ya Mbozi iliyosomwa kwa mgeni  rasmi wamesema kuwa miongoni mwa malengo ya Chama hicho ni kuwalea vijana ili waweze kupambana na maisha yao na kuamsha uzalendo kwa vijana pamoja na kujiwekeza katika miradi mbalimbali ili kujikwamua.


Pia chama hicho kimewaomba viongozi, wadau kuunga mkono juhudi zinazofanywa na chama hicho cha skauti.


Mhitimu wa mafunzo hayo ambaye pia ni mwanafunzi wa kidato cha tano Shule ya Sekondari Vwawa, Beauty Brayton amesema kuwa mafunzo hayo yamewajenga kimwii na kiafya.


"Tumepata mafunzo ambayo yametujenga kimwili na kiafya" 


Amesema kuwa watakwenda kufanyia kazi nasaha  walizopewa na Mkuu wa Wilaya huku wakiwashukuru wote waliosaidia kufanikisha mafunzo hayo.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

UDUMAVU BADO TISHIO -DUGANGE

SONGWE JOGGING WARUDI NA MEDANI ZAIDI YA KUMI NA TANO TULIA MARATHON

MOMBA HAWANA JAMBO DOGO: ROUTE VIONGOZI NA WANANCHI WAKUTANA PAMOJA ROUTER MATCH YANOGA