DC ILEJE AAGIZA KUUNDWA KLABU ZA KUSIMAMIA MAZINGIRA MASHULENI
Katika kuhakikisha jamii inakuwa na elimu endelevu ya uhifadhi wa mazingira wilayani Ileje mkoani Songwe, mkuu wa wilaya hiyo Mhe. Farida Mgomi ameagiza kuundwa Kwa klabu za mazingira kwenye shule za msingi na sekondari Kwa lengo la kuhamasisha uhifadhi wa mazingira.
Mhe.Mgomi ametoa agizo hilo Julai 5, 2023 katika Kijiji cha Chitete kata ya Chitete wilayani humo wakati Dunia ikiadhimisha siku ya mazingira kwa mwaka 2023 iliyobebwa na kauli mbiu; "Tokomeza matumizi ya mifuko ya plastiki" .
Mhe.Mgomi amesema watoto wakijengewa uwezo wakiwa angali wadogo wanaweza kuwa chachu katika uhifadhi wa mazingira, hivyo tutarejesha uoto wa asili uliokuwepo Toka enzi za mababu zetu.
"Hakikisheni hizi klabu zinaundwa Kwa Kila shule kama zilivyo klabu za kupambana na madawa ya kulevya, klabu ya kupambana na rushwa, ili pia klabu ya kupambana na mazingira itakapojengewa uwezo wa kujuwa madhara ya uharibifu wa mazingira utakuwa msaada wa kukabiliana na kutokea Kwa majanga", amesema Mhe.Mgomi.
Mhe. Mgomi amesema Kwa wilaya ya Ileje shule tatu ambazo ni Sekondari ya Msomba pamoja na shule za Msingi Bulanga na Namasele zilizopo kata ya Malangali ndizo shule pekee zenye klabu za mazingira zilizoundwa na halmashauri ya wilaya kwa kushirikiana na Kamisheni ya Bonde la Mto Songwe.
Jumla ya miti 2716 rafiki wa mazingira imepandwa kwenye vyanzo vya maji vya Itumba,Iyela pamoja na Ilumba huku Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) wakigawa miche 16,850 ya miti ya aina mbalimbali

Maoni