DC ILEJE AFUNGA MAFUNZO YA SKAUTI AWACHA NA UJUMBE WA KUPINGA UKATILI
SKAUTI wilayani Ileje Mkoani Songwe wametakiwa kuwa chachu ya uzalendo na kujituma kwenye jamii Kwa kukemea matukio ya ukatili kwa kuripoti kwenye mamlaka husika ikiwepo viongozi wa vijijiji, jeshi la polisi na ustawi wa jamii.
Mkuu wa wilaya hiyo Mhe. Farida Mgomi amesema hayo Juni ,3,2023 wakati akifunga mafunzo ya skauti Kwa vijana 267 yaliyofanyika Kwa siku 5 katika shule ya sekondari Ndola iliyopo kata ya Ndola wilayani humo.
Mhe. Mgomi amewataka skauti hao kuwa mabalozi wa kupinga ukatili Kwa kutumia mafunzo hayo waliyofundishwa kanuni, na taratibu za skauti Kwa lengo la kulisaidia taifa kukabiliana na matukio yasiyo mema Kwenye jamii.
"Ukijifunza mafunzo ya Skauti huwezi kuwa lege lege na ni lazima utakuwa mzalendo na huwezi kukanyagwa na kuwa mkia bali utakanyaga na kuwa kichwa", amesema Mhe.Mgomi.
Mhe. Mgomi amesema tuendelee kuishi na falsafa za mwanzilishi chama cha Skauti Ulimwenguni Sir.Rord Robert Stephenson Smyth "Baden Powell" februari 22 mwaka 1857 Nchini Uingereza ambaye hizi kanuni na taratibu mnazojifunza aliziishi kizalendo na mpaka Sasa zikawe msaada kwenu na jamii ikiwemo kupinga ukatili.
"Natamani kizazi Cha skauti kwenu ninyi ambao Bado ni wanafunzi muendelee kusoma Kwa bidii kwani hatutegemei skauti unafanya vibaya darasani mkizoea hivyo mtakuwa hamziishi kanunui na miongozo ya skauti mliyofundishwa",amesema Mhe.Mgomi.
Kamishina wa Skauti wilayani hapa Imani Joseph Mwakyambiki amesema mafunzo hayo yatawajenga vijana hao kuwa wazalendo kwenye nchi yao kwani wamefundishwa namma ya kusaidia jamii ikiwepo kwenye shughuli za jamii kwa kufuata kanuni na taratibu za mwanzilishi wa Skauti Baden Powell.
Kwa wilaya ya Ileje mafunzo hayo yamewahi kutolewa Kwa mara ya kwanza Kwa shule ya Sekondari Kakoma na Sange hivyo mafunzi yaliyohitimishwa Sasa ni mwendelezo na wanatarajia kuwa na vijana wengi wa shuleni na mtaani ",amesema Mwakyambiki.
Aliko Mlungu amesema wamefurahi kupewa mafunzo hayo ambayo yamewasidia kujuwa kanunui na taratibu zake ikiwemo kuwa wazalendo kwenye jamii na Taifa kwa ujumla.
PICHA ZA MATUKIO MBALIMBALI














Maoni