DC ILEJE AIAGIZA RUWASA KUPELEKA MAJI MAENEO YENYE CHANGAMOTO YA MAJI


MKUU wa wilaya ya Ileje mkoani Songwe Mhe. Farida Mgomi amewataka wananchi kutunza miundombinu ya maji, huku akiagiza wakala wa maji vijijini RUWASA kupeleka maji kwenye vitongoji ambavyo havina huduma hiyo.


Mhe. Mgomi amesema hayo Juni 27,2023 wakati akizungumza na vyombo vya watumia maji kwenye kata ya Ndola, Mlale ,Chitete na Mbebe lengo likiwa ni kuangalia changamoto zinazowakabili wananchi kwenye miradi hiyo.

Mhe. Mgomi amesema serikali imepeleka miundombinu ya maji ,hivyo wananchi hawana budi kuendelea kuitunza Kwa kuchangia Ankara za maji.


"Tupende tusipende lazima tuchangie fedha kwa ajili ya kuendeleza miradi hii ,kwani ipo kisheria, kwani  pesa tunachangia Kwa kaya kuanzia 1500 mpaka 2000 na taasisi kuchangia 3000 hadi 5000", amesema Mhe.Mgomi.


Mhe.Mgomi amemuagiza Meneja wa RUWASA wilayani humo kuhakikisha vile vitongoji ambavyo bado havina maji vipelekewe katika bajeti ya mwaka 2023/2024 ili kuondokana na tatizo hilo.


Sambamba na hilo Mhe. Mgomi amewataka viongozi wa ngazi zote wilayani Ileje kutumia mikutano ya hadhara kutoa elimu ya kutunza miundombinu na vyanzo vya maji ili kuhakikisha wananchi wanapata maji Kwa kipindi Cha mwaka mzima.


Aidha Mhe.Mgomi amesema wananchi waendelee kuhamasishwa umuhimu wa kulipa Ankara za maji ili kufanya matengenezo madogomadogo na kuweza kusogeza mitandao ya mabomba kwenye maeneo yao.








Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE