DC MAHAWE AONYA WANAOHARIBU VYANZO VYA MAJI



Mkuu wa Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe, Esther Mahawe amewaagiza wananchi wa wilaya hiyo kutunza mazingira ikiwemo vyanzo vya maji ili kuwaponguzia adha wanawake ya kutafuta maji umbeli mrefu.


Mkuu huyo wa Wilaya ametoa maagizo hayo leo Jumatatu Juni 5, 2023 wakati akizungumza katika Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ambayo kiwilaya yamefanyika Kijiji cha Nambala kata ya Mlowo wilayani humo.


Amesema kuwa maji yanapokuwa changamoto wanawake na watoto ndio wanaathirika kwa kiasi kikubwa hasa kwa kutafuta nishati hiyo.


"Msisahau kuwa maji yanapokuwa changamoto wanamama na watoto ndio wanapata shida kwenda kutafuta maji" 

Amesema lengo la Rais Samia Suluhu Hassan ni kumtua ndoo mama kichwani kwa kuwasogezea huduma ya maji karibu ili muda wanaotumia kutafuta maji wautumie kwenye shughuli za uzalishaji.


"Maelekezo niliyotoa yazingatiwe, tutunze vyanzo vya maji". 


DC huyo amesema kuwa wilaya hiyo ina bahati ya kuwa na vyanzo vingi vya maji lakini changamoto moja ni kubwa iliyopo ni kutokutunza vyanzo hivyo.


"Hali ya maji kwa wilaya ya Mbozi ikiwa hatutalinda vyanzo hivi miaka isiyozidi 10 tukienda hali hii tutakosa maji" amesisitiza


Amewataka wanaolima kwenye vyanzo vya maji kuacha tabia hiyo kwa kuwa ndio chanzo cha kukausha vyanzo hivyo.


"Hali ya upatikanaji wa maji sio nzuri. Mnaweza msiione leo lakini siku zinakuja mtaomboleza. Maji hayana mbadala. Tutunze hivi vyanzo" ametahadharisha mkuu huyo wa wilaya.


"Babu zetu wasingevitunza hivi vyanzo sisi tusingevikuta, kila mtu akilima kwenye vyanzo vya maji pakikauka tutakwenda kulima wapi" amehoji DC huyo.


Katika maadhimisho hayo yaliyoongozwa na mkuu wa wilaya, miti 1000 imepandwa katika chanzo cha maji cha Nambala.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

UDUMAVU BADO TISHIO -DUGANGE

SONGWE JOGGING WARUDI NA MEDANI ZAIDI YA KUMI NA TANO TULIA MARATHON

MOMBA HAWANA JAMBO DOGO: ROUTE VIONGOZI NA WANANCHI WAKUTANA PAMOJA ROUTER MATCH YANOGA