Wanafunzi wa vyuo vya kati kuanza kupata mikopo mwaka huu

 Serikali imependekeza kuanzishwa kwa programu ya mikopo ya wanafunzi waliochaguliwa katika vyuo vya kati katika fani za kipaumbele ambazo ni sayansi, afya, uchumi na ualimu.




Waziri wa Fedha na Mipango Dk Mwigulu Nchemba ametoa pendekezo hilo leo bungeni wakati akiwasilisha bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2023/2024.



Amesema hatua hiyo inalenga kuongeza idadi ya wataalamu na ujuzi unaohitajika katika azima ya mapinduzi ya viwanda.


Waziri Mwigulu pia amesema wanapendekeza kuondolewa ada kwa wanafunzi wa   kidato cha nne ambao watapangiwa na Serikali kwenda kujiunga na vyuo vya ufundi vya Dar es Salaam, Mbeya na Arusha Tech.


Kwa mujibu wa waziri huyo, hatua hiyo inalenga kuongeza idadi ya wataalamu wenye ujuzi na elimu inayohitajika katika zama hizi za mapinduzi ya nne ya viwanda.


“Nilisema hotuba hii imebeba hotuba ya Mama namna anavyotaka kuwasaidia watoto wa maskini. Pochi ya Mama imefunguka. Mama yuko kazini,” amesema Waziri Mwigulu.


Amesema kutokana na mabadiliko ya Sera ya Elimu na mitaala ambapo Serikali inalenga kutoa elimu ya amali kwa ngazi zote, elimu itakayomuwezesha kijana wa Kitanzania kujiajiri au kuajiriwa, Serikali inapendekeza kuanzisha programu ya mikopo kwa wanafunzi wanaochaguliwa na Serikali kusoma kwenye vyuo vinavyotoa elimu katika fani za kipaumbele.”


Amezitaja fani hizo ni sayansi, afya, ufundi na ualimu. “Hatua hii itaanza na wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa masomo wa 2023/24…pia Mama aliamua kuongeza kiwango cha posho ya kujikimu maarufu kama ‘boom’kwa wanafunzi wa Elimu ya Juu kutoka Sh8,500 hadi Sh10,000 kwa siku.”

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE