KAMATI YA SIASA SONGWE YAISIFU WILAYA YA SONGWE KWA KUISIMAMIZI MZURI WA MIRADI

 


Kamati ya Siasa Mkoa wa Songwe imeanza Ziara ya kukagua miradi Mbalimbali inayotekelezwa na Serikali ambapo Kamati hiyo imeanza na Miradi ya Wilaya ya Songwe.Ikiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Songwe Ndugu Radwell Mwampashi imeweza kugagua jumla ya Miradi saba Halmashauri ya Songwe.


Katika Ziara hiyo Kamati hiyo imekagua Miradi ya Afya, Barabara, Maji na Miundo mbinu ya Shule ambapo Kamati imeridhika na Usimamizi na Ujenzi wa Miradi hiyo Wilaya Songwe na Kuwapongeza Viongozi wa Songwe wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Solomoni Itunda.


Wakiongea kabla ya kuhitimisha Ziara hiyo Wajumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa Mnec Mkoa wa Songwe Aden Mwakyonde amesema Wilaya ya Songwe Wamejitahidi sana kuisimamia Miradi inayotekelezwa chini ya Ilani ya CCM na wanastahili Pongezi huku akimtupia sifa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Songwe CPA Cecilia Kavishe kwa kuwa mfuatiliaji wa miradi hiyo na kumtaka kuendelea hivyo katika Miradi mingine iliopo na itakayokuja Wilayani Songwe.


Kwa Upande wake Mjumbe mwingine wa Kamati hiyo Dkt Fransis  Michael ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe amewapomgeza Uongozi wa Wilaya hiyo pia akianza na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mhe Abraham Sambila kwa niaba ya Madiwani wote wa Wilaya hiyo kwa kuendeleza umoja na mshikamano wao wa kuijenga Wilaya Songwe.


Akihitimisha Mwenyekiti wa Kamati Ndugu Radwell Mwampashi ametoa pongezi kwa Ujumla Viongozi wote wa Songwe kwa ushirikiano wanaouonyesha Wilaya hiyo.


"Hii Miradi ni Utekelezaji wa Ilani ya CCM  mkiiharibu CCM itashindwa kujibu kwa Wananchi wake sasa Wilaya ya Songwe niwapongezeni sana kwa usimamizi huu mzuri na pia kwa umuhimu wake nimpongeze Mbunge wa Songwe  Mheshiwa Philipo Mlugo kwanza kwa uwepo wake katika Ziara yetu hii ya leo na pili kwa kuhakikisha fedha zinakuja za miradi mikubwa katika Wilaya hii ya Songwe huyu ni Mbunge mchapa kazi na kazi anaijua"amesema Mwampashi


Aidha Mwenyekiti amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuitekeleza Ilani ya CCM kwa Vitendo na ameshukuru kwa niaba ya Wananchi wa Songwe kwa kuipatia Wilaya hiyo Fedha za Miradi mbalimbali ya Wilaya ya Songwe huku akimuahidi kuwa 2025 pasi na shaka kura za kutosha zitatoka kwa Wananchi wa Mkoa wa Songwe. Ziara hiyo inaendelea katika Halmashauri zingine nne za Mkoa wa Songwe

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE