MAWAKALA WAPIGWA MARUFUKU KUINGIZA LORI FOLENI LISILO NA NYARAKA
Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Dkt. Francis Michael amewapiga marufuku mawakala kuingiza malori foleni yanayovuka mpaka wa Tunduma kama hawajakamilisha nyaraka za kuvuka ili kuondokana na foleni isiyokuwa ya lazima katika mji wa Tunduma.
Mkuu wa Mkoa amepiga marufuku hiyo akiwa na mawakala hao ofisini kwake baada ya kupokea taarifa ya kamati aliyounda mnamo 14 Juni 2023 ya kuchunguza kwa kina sababu zinazochangia foleni kubwa ya Malori katika mji wa Tunduma na kubaini Malori mengi yanakuwa foleni wakati hayana nyaraka.
"Nyie mawakala ndio mnaruhusu malori yaingie foleni na nimepata taarifa kuna watu foleni isipokuwepo hawana rahaa sasa kuanzia leo lori ikikutwa foleni haina nyaraka wakala uyo atachukuliwa hatua kali" Mhe. Dkt. Francis Michael.
Mkuu wa Mkoa, Mhe. Dkt. Francis Michael amesema kitendo cha mtu moja kusababisha foleni bila sababu za msingi ni sawa na kosa la uhujumu uchumi, hivyo amewataka mawakala kuacha tabia hiyo.
"Kamati niliyounda imeweza kupitisha magari zaidi 700 kwa siku moja na hali ya Tunduma Barabara zinapitika hii inaonyesha kabisa Tunduma bila kuwa na foleni inawezekana tukiacha ujanja ujanja" Mhe. Dkt. Francis Michael.
( MENEJA TANROADS ENG SULEIMAN BISHANGA AKIWA NA TIMU ILIONDWA KUSHUGULIKIA SUALA LA FORENI TUNDUMA)Mwenyekiti wa madereva Tanzania, Ndg. Schubert Mbakizao ambaye pia ni Balozi wa Bandari amesema kila mtu kwa sehemu yake akitekeleza majukumu yake mpaka wa Tunduma haupaswi kuwa na foleni.
"Dereva anakuja na nyaraka kwenye foleni tunaomba mawakala nao wazipeleke nyaraka izo sehemu husika, Jeshi la Polisi lifanye majukumu yake, TRA nao watimize majukumu yao Tunduma haiwezi kuwa na foleni" Schubert Mbakizao.
Jones Rugonzibwa kutoka kampuni ya RHG ameiomba Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) kuimarisha uhusiano na mawakala waliopo Tunduma kwa kuwa mawakala wanafanya kazi kwa ukaribu na TRA hivyo wao wakiaribu itaonekana ni TRA wamearibu, hivyo ushiriki unahitaji kutatua foleni ya Tunduma.
Nuhu Mgodoka-Mwenyekiti wa chama cha wafanyakazi wa Malori Nyanda za juu kusini.(CHAMAWATA) ameishukuru Serikali kwa hatua ambazo wamechukua kuhakikisha madereva hawana shida kwa sababu adhaa ya foleni mwisho anayeumia ni dereva.
Comments