MENEJA TANESCO SONGWE AIKOSHA KAMATI YA SIASA SONGWE YAMPONGEZA KWA USIMAMIZI WA MIRADI YA REA
Mradi wa Umeme wa REA Kijiji cha Rungwa kata ya Isansa umeleta furaha ndani ya Kijiji hicho kiasi kwamba hali ya kiuchumi ndani ya Kijiji hicho imedaiwa kukua kwa kasi.Ziara ya Kamati ya Siasa Mkoa wa Songwe ukaguzi wa Miradi Wilaya ya Mbozi ikiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Songwe Radwell Mwampashi pamoja na Kamati ya Siasa Wilaya Mbozi imeupongeza Mradi huo na pia kumshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassani kwa kukikumbuka Kijiji cha Rungwa na kukipelekea mradi huo wa Umeme.
Wakiongea mbele ya Kamati hiyo Wananchi wa Kijiji hicho wameupongeza Mradi wa REA na kukiri wazi kijiji chao kimeneemeka na Umeme na wameanza kuona mabadiliko ndani ya kijiji chao hali inayopelekea uchumi wao kupanda.
"Mwenyekiti naona niishukuru Serikali kwa kutuletea Mradi huu ndani ya Kijiji hiki hata shughuli za kimaendeleo tunaona ukuaji wake leo tuna mita za mashine hapa kijijiji kiukweli kwa namna ya pekee niwapongeze sana" Amesema Joshua Mwamlima mkazi wa Rungwa.
Nae Mwenyekiti wa kijiji Bahati Msongole hicho licha ya kushukuru ameuomba Uongozi wa Tanesco kuwasaidia nguzo zingine 40 walizozileta waweze kuzielekeza katika Vitongoji vya Kijiji hicho ambapo Meneja wa Tanesco Mkoa wa Songwe Mhandisi Narowil Sabaya amemsema Mkoa wa Songwe jumla ya Vitongoji 151 vitanufaika na mpango wa Serikali wa mradi jazilizi (Densification) ambao unaanza mwezi wa Nane hivyo Vitongoji vilivyomo ni pamoja na vya Vitongoji vya Vijiji hicho.
Kabla ya kuitimisha ukaguzi Mwenyekiti Mwampashi aliwataka Wajumbe wa Kamati hiyo kuchangia ambapo Mjumbe Ranson Mwaipula ambae ni Mwenyekiti Mkoa Wazazi alimpongeza Meneja wa Tanesco Mkoa wa Songwe Mhandisi Narowil Sabaya na kusema uwezo wake wa kikazi ni mkubwa na Mkoa wa Songwe umepata Mwandishi mzuri hivyo ana imani Miradi mingi ya Tanesco inafanikiwa kutokana na juhudi za usimamizi wa Meneja huyo
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Fransis Michael Mjumbe wa Kamati hiyo aliwaomba Tanesco pindi wakikabidhiwa mradi huyo wahakikishe wanaongez idadi ya watu kuunganishiwa Umeme na ikibidi wabadilishe transfoma iliopo hapo.
Akihitimisha Mwenyekiti Mwampashe amesema Ilani ya Uchaguzi 2020 imeahidi kila kijiji kupata umeme hivyo Rais Dkt Samia Suluhu anastahili pongezi za dhati kwa kutekeleza Ilani kwa Vitendo na kusema huko ndio maana ya Chama na Serikali
"Ndugu zangu mimi kama mwenyekiti wa chama na Mwwnyekiti wa Kamati hii naomba nimpomgeze Meneje wa Tanesco Songwe ni jembe huyu mama na jasiri kwa ujembe wake Mkoa huu utafika mbali tumtumie Vizuri na tumesemee kwa mazuri" amesema Mwampashi
Kamati hiyo inatarajia kuhitimisha Ukaguzi wa miradi kati halmashauri ya Tunduma
Comments