MLEMAVU APEWA MSAADA NA DC MBOZI

 

ANAADIKA MKUU WA WILAYA MBOZI  MHE ESTER MAHAWE JUU YA KIJANA MWENYE ULEMAVU

Leo Asubuhi Tarehe 26.06.23 nimetembelewa na mgeni anayefahamika Kwa Jina la Kevin Danken Haonga mkazi wa kijiji cha Mahenje Kata ya Mahenje Wilaya ya Mbozi mwenye ulemavu wa miguu. Huyu rafiki yangu anahitaji msaada wa baiskeli ya miguu mitatu Kwa kuwa mikono yake iko Sawa ili aweze kutoka eneo moja kwenda kingine na kujitafutia mahitaji yake. Kevin ana umri wa miaka 19 na hakubahatika kusoma. Kevin ni Mtoto wa tatu katika familia ya watoto 6 wa Mzee Danken Haonga. Kati yao wenye ulemavu kama wa kwake ni watatu. Kaka yake mwenye umri wa miaka 22 aitwaye Jackson pamoja na mdogo wake mwenye umri wa miaka 2.

      Kwa bahati njema nimempatia Kevin baiskeli kutoka Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ileje Mhe. Farida Mgomi . Mwenyezi Mungu ambariki Sana Dada yangu katika kazi. Lakini pia Kwa kuwa Kevin anatamani kusoma, nimeelekeza apelekwe shule ya watu wenye mahitaji Maalum ya Mwenge Kwa msaada wa Afisaelimu Msingi ili Naye aweze kutimiza ndoto yake na akishajua kusoma atajiunga na mfumo wa IPOSA ili aweze kujifunza fundi wowote atakaoupenda yeye Kulingana na Aina ya ulemavu wake. Kwa kuwa Kevin anatokea kwenye familia za hali ya chini kinaisha,ikiwa MTU yoyote ataguswa ili apate mahitaji binafsi awapo shuleni,unaweza kuwasilisha msaada wako kupitia Kwa Kaimu DAS ndugu Lugongo Kwa namba 0742202987  ama moja Kwa moja shuleni Mwenge baada ya Kevin kuanza Shule Jumatatu ijayo.


Ni Imani yangu kuwa Ofisi ya ustawi wa Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi  itahakikisha watoto wote wenye ulemavu wanaoweza kwenda shule wanapelekwa shule. 

Tuwapende,Tuwathamini Tuwasaidie ili nao wazitimize ndoto zao. 

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE