MOMBA WAANZA KUJENGEWA LAMI KILOMITA 17,WAMPONGEZA RAIS DKT SAMIA
Wakazi wa Wilaya ya Momba wamefurahia Ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami itakayoanzia Utambalila hadi Round about Chitete kata ya Chitete ambapo zipo ofisi za Wilaya ya Momba.Barabara hiyo inayojengwa chini ya Usimamizi wa Wakala wa barabara Tanroads kupitia kampuni ya (JNMS) imeshaanza kujengwa mji wa Tindingo.
Kaimu Meneja Tanroads Mkoa wa Songwe Mhandisi Suleiman Bishanga amesema Ujenzi wa barabara hiyo umeanza eneo la Tindingoma na Mkandarasi yupo eneo la kazi muda wote kuhakikisha muda aliopangiwa kumaliza unafanyika kwa wakati na itajengwa kilomita 17 kutoka Chitete hadi Utambalila.
"Niwaombe wakazi wa Momba kuhakikisha wanazitunza barabara hizi kwani Rais wetu Dkt Samia Hassan ametoa fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa barabara hizi hivyo kuziharibu au kuiba miundo mbinu ni kuiokosea serikali hivyo natoa rai kwa Wananchi kuzitunza hizi barabara" amesema Bishanga
Aidha Bishanga amesema Tanrods wataweka pia taa barabara hiyo ili kurahisha shughuli za kiuchumi kufanyika muda wote.
Pascal Simkonda mkazi wa Tindingoma amemshukuru Rais Samia kwa kuwasikiliza kilio chao Wakazi wa Momba kwa kuwaletea miradi mikubwa ya afya, barabara, Maji na mingine mingi na amesema kwa ujenzi wa barabara hiyi kwao ilikuwa ni ndoto kuiona lami lakini kwa awamu hii ya sita imewatendea miujiza
Nae Mkurugenzi wa halmashauri ya Momba Regina Bieda amewapongeza Tanroads chini ya Meneja wao Bishanga kwa kuijali Momba na kuwaletea mradi huo unakwenda sambamba na Ujenzi wa ofisi za Halmashauri hiyo lakini pia sambamba na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Momba na ofisi zingine
"Tanroads wametukosha sana Momba mji umeanza kubadilika kabisa hata mandhali yake imebadilika sasa kiukweli tuwape sifa zao na hii barabara ikikamilika itaturahishia sana kuingia na kutoka Chitete hivyo shughuli za kijamii zitafanyika kwa haraka sana" amesema Bieda
Comments