MRATIBU WA MAANDAMANO DAR HAJATOKEA WENZIO WADAKWA NA POLISI

 


Dar es Salaam. Jeshi la Polisi limewakamata baadhi ya vijana waliojitokeza kuandamana kupinga mkataba wa ushirikiano wa uendeshaji wa bandari kati ya Kampuni ya DP World na Tanzania.


Hata hivyo, mratibu wa maandamano hayo, Deus Soka katika hali ya kutofahamika, hajatokea kwenye maandamano hayo yaliyopangwa kuanzia Temeke na kuishia Ikulu, jijini Dar es Salaam.


Mwananchi Digital ilipomtafuta kwa simu zake zote za kiganjani, hakupatikana na katika majina ya waliokamatwa na polisi pia jina lake halikuwepo.

Juni 15 mwaka huu Deus Soka ambaye aligombea udiwani katika Uchaguzi Mkuu wa 2020, alitangaza kuitisha maandamano kupinga mkataba wa ushirikiano wa uendeshaji wa bandari kati ya Kampuni ya DP World na Tanzania.


Hata hivyo Juni 17 Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam likipiga marufuku maandamano hayo na kueleza kuwa, mtu aliyeandaa maaandamano hayo ameshajibiwa kwa barua akielezwa ni marufuku kufanyika maandamano yoyote.


Maandamano hayo yalipangwa kuanzia Temeke kwenda Ikulu ya magogoni kupitia maeneo mbalimbali ikiwemo Keko, Karume, Kariakoo na Mnazi Mmoja lakini leo asubuhi walibadilisha na kutangaza kuanzia Mnazi Mmoja.


Mwananchi Digital likizunguka maeneo mbalimbali na kushuhudia vijana wakiwa makundi makundi huku gari za polisi zikizunguka maeneo mbalimbali.


Hata hivyo wakati Polisi na vijana hao wakiendelea kuwindana ghafla walijitokeza na kuingia barabarani wakiwa na mabango lakini hatua chache baadaye walikamatwa.


Juni 10, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilipitisha azimio kuhusu pendekezo la kuridhiwa kwa mkataba baina ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai kwa lengo la kuanzisha ushirikiano katika uendelezaji wa maeneo ya bandari nchini.


Pendekezo hilo liliwasilishwa bungeni Juni 10, na kupitishwa na Bunge baada ya wabunge kupata fursa ya kuchangia na kuishauri Serikali kuhusu mkataba huo.

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE