UJENZI JENGO LA MKURUGENZI MOMBA SI WA KITOTO MKURUGENZI AWASHANGAZA KAMATI YA SIASA MKOA
Ujenzi wa jengo la Utawala halmashauri ya Momba unaendelea katika hatua za Mwisho Makao Makuu wa Wilaya hiyo Chitete umesifiwa na Kamati ya Siasa Mkoa wa Songwe ikiongozwa na Mwenyekiti wake Radwell Mwampashi.Ikiwa ni siku ya pili ya Ziara kamati katika Ukaguzi wa Miradi Mbalimbali inayotekelezwa na Serikali ya awamu ya Sita chini yake Rais Dkt Samia Suluhu Hassani
Mara baada ya Ukaguzi wa Maradi huo Mkubwa Wilayani Momba wenye gharama ya........ Wajumbe wa Kamati hiyo walimpongeza Mkurugenzi wa Halmashauri Regina Bieda kwa kusimamia vyema Ujenzi wa jengo hilo na kuhakikisha fedha ya serikali inatekelezwa kwenye Mradi kama ilivyopangwa lakini pia kuhakikisha kile kilichokusudiwa ndicho kinachotekelezeka
"Kwa ujumla Mradi huu ni mzuri na kwa kuangalia tu umetekelezwa kwa kiwango kizuri na kamati ya Siasa hatuna shaka na Mradi huu kiukweli tukupongeze Mkurugenzi wa Momba na timu ya Wataalamu wako wote kwa Usimamizi wa Jengo hili la kisasa kabisa na lenye ubora" alisema Mwenyekiti CCM Mkoa wa Songwe Radwell Mwampashi
Aidha Mwampashi amesema taswira ya Mji wa Chitete imebadilishwa na Ujenzi wa Miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali na kuwataka Wana Momba kuhakikisha wanaitunza Miradi hiyo na kuilinda kwa Serikali imetua gharama kubwa kuijenga hivyo inahitaji kutunzwa
Comments