VIBANDA VYATEKETEA NA MOTO SOKO LA MLOWO CHANZO CHADAIWA JIKO LA KUKAANGIA SAMAKI


 Moto umeteketeza baadhi ya Vibanda katika soko la Magwaza lililopo Mlowo Wilayani Mbozi usiku wa jana  Jumamosi.


Kwa mujibu wa mashuhuda wa moto huo wamedai chanzo cha moto huo kinaweza kuwa jiko la kuni ambalo hutumiwa na mama mmoja anaejihusha na ukaangaji wa Samaki.

John Kabuje ambae anaishi jirani na soko hilo amedai kuwa usiku wa saa tatu kasoro usiku ndio moto huo ulipoanza kuibuka na ulianzia kwenye banda la mama mkaanga samaki na hatimae kushika vibanda vingine.


"Bahati nzuri walikuwepo baadhi ya wateja wa vinywaji vya kilevi walikuwa wanakunywa ndani ya soko hili waliwahi kuona moto huo kabla haujaleta madhara makubwa"alisema shuhuda Kabuje


Kwa upande wa Mwenyekiti wa soko hilo Tumaini Kabuje amesema chanzo cha moto huo ni jiko la samaki na jumla ya vibanda vilivyoathirika ni  vitatu pamoja cha kibanda chenyewe cha Mama muuza samaki


Aidha Mwenyekiti huo amesema kuwa kumekuwepo na tabia  baadhi ya wakaanga samaki sokoni hapo kukaangia samaki wao ndani ya vibanda vya mbao hali ambayo ni hatarishi sokoni hapo endapo kukitokea madhara kama hayo yaliotokea jana.


"Hatua za awali baada ya hili tukio  kama Viongozi wa soko tunapiga marufuku shughuli zote za ukaangaji samaki ndani ya Vibanda na ufanyike nje ya vibanda  hatua na gharama za waathirika wa kuunguliwa vibanda vyao tutatoa maamuzi baada ya kikao chetu Viongozi" amesema Tumaini

Vibanda vilivyoathiri ni vitatu ambavyo vinamilikiwa na  Joseph Mwamahonje kingine Mmiliki wake ni Nuru Kayuni na Mama Amosi ambae ni mkaanga samaki jiko ambalo ndio linadaiwa chanzo cha moto huo

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

KUMBUKUMBU YA MAISHA YA MH. ESTER ALEXANDER MAHAWE

CONSTRUCTION OF THE ISONGOLE-ISOKO ASPHALT ROAD IS NOW OFFICIAL, CONTRACTOR INTRODUCED TO THE PUBLIC

*KUNDO AGOMA KUWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA MAJI VWAWA-MLOWO