CCM SONGWE YARIDHISHWA NA MIRADI YA TARURA WAPONGEZWA


 Kamati ya Siasa Mkoa wa Songwe ikiongozwa nae Mwenyekiti wa CCM Mkoa Radwell Mwampashi  imefanya Ukaguzi wa Miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali ya awamu ya sita Chini ya Dkt Samia Suluhu Hassan ambao ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi.


Katika Ziara hiyo kamati imeweza kukagua miradi Tarura Ujenzi wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Songwe ikiongozwa nae Mwenyekiti wa CCM Mkoa Radwell Mwampashi  imefanya Ukaguzi wa Miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali ya awamu ya sita Chini ya Dkt Samia Suluhu Hassan ambao ni utekelezaji wa Ilani.

      ( Ujenzi wa barabara kiwango cha lami Kiwila-landani Wilayani Ileje)

Katika miradi ya barabara inayotekelezwa na Wakala wa barabara Vijijini na Mijini (Tarura) jumla ya Miradi mitano imeweza kukaguliwa na Kamati ambapo pamoja na kuikagua kamati imewapongeza Tarura kwa kuweza kusimamia Vyema miradi ya barabara Vijijini Mkoani Songwe na kuishauri kurekebisha palipo na kasoro ndogo ndogo.


Wakitoa maoni yao Wajumbe wa kamati hiyo waliwapongeza Watendaji wa Tarura wakiongozwa na Meneja Mkoa wa Songwe Tarura Mhandisi Kiliani Haule ambapo Wajumbe wamesema hali ya barabara nyingi za Vijijini zinaridhisha hivyo inadhihirisha kuwa Usimamizi wa miradi Tarura ni wazuri

 ( Ukaguzi barababara ya Sogea- Mpande)

Jobu Kabinji  Mjumbe wa Kamati amesema barabara za Tarura ndani Mkoa wa Songwe zinaridhisha hivyo amewataka Tarura pia kuziangalia barabara zingine za Mkakati kwa jicho la pili ili nazo ziweze kupitika kiurahisi


Fatuma Yusuph Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Songwe ambae pia ni Mjumbe wa Kamati ya Siasa amewashukuru Tarura kwa kuwajali Vijana na kuwapa kazi za Ujenzi katika Miradi mbalimbali inayotekelezwa Mkoani Songwe hivyo amewaombe kuendelea kutoa ajira kwa Vijana wengine walioko miradi inakupita kwani kufanya hivyo ni kuongeza ajira kwa Vijana wasio na ajira isio rasmi


Akihitimisha Mwenyekiti CCM Radwell Mwampashi amewataka Tarura kuzingatia uchepushaji wa maji kwa kujenga mitaro na kuilekezea sehemu sahihi na isiwe kwenye makazi ya watu


"Nina kila sababu ya kuwapongeza Tarura kiukweli kwenye kujenga barabara hapana tuwape tu sifa zenu Tarura mmetisha sana labda niwaombe tu kitu kimoja mnapojenga barabara hizi hakikisheni mitaro hailekezwi kwenye makazi ya watu ili maji yasije leta madhara kwa watu na makazi yao" amesema Mwampashi


Katika Ziara hiyo kamati imeweza kukagua miradi Tarura Ujenzi wa barabara  Kiwila - Landani uliopo Ileje wenye thamani ya shilingi 5,752,956,420 mradi mwingi uliotembelewa ni barabara ya

 Sogea - Mpande iliopo Tunduma inayojengwa kwa gharama ya shilingi 470,065,360 barabara nyingine ni 

 Mkwajuni Wilayani Songwe na gharama ya mradi ni shilingi 500,000,000

barabara ya Ilolo - Ndolezi Iliopo Mbozi gharama ya shilingi 6,465,596,070 na Daraja la chuma lililopo Momba yenye gharama ya shilingi 338,000,000 kamati imemaliza Ziara yake


Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE