DIRA YA MAENDELEO TAIFA 2050 YAJADILIWA SONGWE
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Dk Fransis Michael ameongoza Semina ya Mafunzo elekezi ya maandalizi ya dira ya taifa ya maendeleo 2050 kwa watumishi wa Umma katika ukumbi wa Mkoa uliopo katika jengo la ofisi yake Wilayani Mbozi.
Akiongea katika ufunguzi Mkuu wa Mkoa amewataka wajumbe wa Semina hiyo iliowashirikisha wakuu wa Wilaya, Madas,Wakurugenzi wa halmashauri, Wakuu wa wa taasisi za fedha,Mameneja taasisi za Umma Viongozi wa Dini, Viongozi wa vyama vya Siasa na Wataalamu mbalimbali toka ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe kusikiliza na kutoa maoni yao kwani ndio dira ya maendeleo ya Taifa hivyo kutoa kwao maoni ndio mafanikio ya Nchi.
( Meneja Tanroads na Meneja Tanesco wakifuatilia kwa makini semina hiyo)"Niwaombe Viongozi wenzangu leo tumepata ugeni toka Wizarani kwa lengo la kutoa semina ya dira ya maendeleo kwa ustawi wa Nchi yetu hivyo tuwasikilize na kutoa maoni yetu kwani ni muhimu sana katika kulipeleka taifa letu mbele"amesema Dkt Michael
Semina hiyo ya maandalizi ya dira ya maendeleo ya Taifa 2050 imefanyika siku moja ambapo wadau mbalimbali waliweza kuchangia
( Wakuu wa Wilaya Mkoani Songwe na Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa wa Songwe)
Mkuu wa Wilaya ya Mbozi Ester Mahawe ameitaka dira ya maendeleo 2050 iangalie suala zima la kilimo kwani jitihada kubwa zimeonyeshwa na serikali ya awamu ya sita kwa kuhimiza Vijana kujiajiri katika kilimo na wameanza na program ya BBT hivyo makundi mengine nayo yahamasishwe katika kilimo
Nae Sheikh wa Mkoa wa Songwe ambae pia ni Mwenyekiti wa kamani ya Amani Mkoa wa Songwe amesema uhuru wa kujieleza uendane na dira ya maendeleo 2050 hivyo uhuru usiokuwa na mipaka huo sio uhuru
"Haiwezekani mtu atumie uhuru huu wa kujieleza kwa kuwatukana Viongozi hadharani, kuwabeza wakati Viongozi hao hao wapo kupanga maendeleo ya Taifa lakini leo tunawatukana hadharani mpaka Mkuu wa Nchi tunamtukana huu sio uhuru katika mipango hii lazima kuwe na ukomo wa uhuru ili kuheshimiana maana sisi katika dini tunaamini Serikali uliopo madarakani imeletwa na Mungu na Viongozi walioko madarakani wanapaswa kuheshimiwa" amesema Sheikh Batuza
Nae Mkuu wa Wilaya ya Ileje Farida Mgomi amesema dira hiyo iipe kipaumbele suala la vyama vya ushirika na kuviwekea mikakati maalumu 2025 ili kuwawezesha na kuwainua wananchi kiuchumi
Wizara ya fedha imetoa semina ya mafunzo kwa Watumishi wa Umma Mkoani Songwe juu ya namna ya kutoa Elimu kwa Wananchi wanaowaongoza juu ya Nini maana ya Dira ya Maendeleo ya Taifa 2020 na 2050 na ni Wapi Taifa linaelekea
Mtoa mada Bi Rosemary Taylor amesema dira ya maendeleo 2025 imesaidia Taifa kuingia uchumi wa kati 2020 hivyo ni vyema sasa taifa kupanga dira mpya ya 2050 ili kujiweka sehemu nzuri kama Taifa
Comments