MBUNGE CHADEMA AKOSHWA NA UTAWALA WA RAIS SAMIA AMMWAGIA SIFA

 Mbunge wa Viti Maalum Jesca Kishoa amesema Tanzania imejaliwa kuwa na Rais mvumilivu asiye na mfano.



Kishoa ambaye ni mbunge kutoka kundi la wabunge 19 wenye kesi mahakamani na uongozi wa Chadema, ametoa kauli hiyo leo Jumapili Julai 23, 2023 kwenye mkutano wa kanda wa CCM unaofanyika uwanja wa bombadia mjini Singida.


Mkutano huo unaongozwa na Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo ukibeba kauli mbiu ya ‘Uwekezaji kwenye bandari ni ufunguo muhimu Kwa uchumi na Maendeleo yetu’ ulihudhuriwa na wana CCM wa Mikoa ya Dodoma, Tabora na Wenyeji Singida.


"Mungu ametupendelea kutupa Rais mvumilivu sana, mama huyu ametupa heshima kubwa sisi wanawake na ninaomba kila mahali mama huyu tumuombee," amesema Kishoa.


Ametaja baadhi ya mambo ambayo amedai Rais Samia ameiheshimisha nchi ni sekta za madini na utalii kwamba zimekuwa zikifanya kazi.


Mbunge huyo amepandaa jukwaani akikaribishwa na Mbunge wa Ukonga, Jelly Silaa na alipopanda jukwaa aliwasalimu washiriki wa mkutano kwa salamu ya kidumu Chama Cha Mapinduzi ambayo ndiyo salamu za chama hicho.


Hata hivyo siyo mara ya kwanza Kishoa kumsifia Rais Samia Suluhu Hassan kwani katika mkutano wa bunge uliokwisha alipeleka bungeni wageni mara mbili ambao walitambulishwa kama ‘chawa wa mama’.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

UDUMAVU BADO TISHIO -DUGANGE

MBUNGE MOMBA KUTOA SHILINGI MILIONI 28 UJENZI WA OFISI ZA CCM KATA 14

BARAZA LA MADIWANI LAWAPONGEZA WALIMU UFAULU WA DARASA LA SABA