MKURUGENZI TUNDUMA ATANGAZA MIKAKATI ZAIDI KUINUA MAPATO YA NDANI.

HALMASHAURI ya Mji Tunduma, Wilaya ya Momba, Mkoani Songwe ipo kwenye mchakato wa kufanya upanuzi wa Maegesho (Truck’s Parking) ya magari makubwa yanayovuka mpaka wa Tanzania na Zambia, kutoka magari 120 hadi malori 300 kwa lengo la kusisimua na  kuiongezea Halmashauri hiyo mapato yake ya ndani.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Philemon Magesa, katika mahojiano maalum na gazeti hili yaliyolenga kupata taarifa zinazohusiana na utekelezaji wa mikakati ya ukusanyaji wa mapato ya ndani na kusababisha mapato hayo kuongezeka mara dufu.

Moja ya Malori ya Mizigo likiingia kupaki katika maegesho ya Halmashauri ya Tunduma. 

Halmashauri ya Mji Tunduma imeongeza wigo wa ukusanyaji wa mapato ya ndani kutoka katika vyanzo vyake mbalimbali, ikiwemo miradi ya kimkakati na kufikia kiasi cha shilingi bilioni 13.7 kwa mwaka.


Akifafanua zaidi kuhusu utekelezaji wa mradi huo wa upanuzi wa maegesho ya magari makubwa yanayovuka Mpaka wa Tanzania na Zambia (Truck’s Parking), Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Magesa alisema  utaongeza  ukusanyaji wa mapato  ndani kutoka shilingi milioni 100 hadi kufikia shilingi milioni 300 kwa mwaka katika chanzo hicho.

Baadhi ya abiria wakiwa wamepumzika kwa kuangalia vipindi mbalimbali katika Tv zilizofungwa eneo la mapumziko la Stendi ya Tunduma. 

“Manufaa ya kutanuliwa kwa mradi huu wa Maegesho kutoka magari makubwa 120 hadi 300 yanayovuka Mpaka wa Tanzania na Zambia (Truck’s Parking) ukikamilika unatarajia kuiongezea Halmashauri hii mapato kutoka mapato ya awali ya shilingi milioni 100 kwa mwaka hadi kufikia  Shilingi milioni 300 lakini pia tunatarajia kujenga nyumba ya kupumzikia hawa madereva na sehemu ya kupata chakula ili wakija vyote waweze kumalizia hapa hapa”.

    (Daladala zikishusha na kupakia abiria Stendi kuu Tunduma iliopo Mpemba)

“Halmashauri hii ina vipaumbele mbalimbali katika utekelezaji wa shughuli zake za kila siku na kipaumbele namba moja kabisa ni ukusanyaji wa mapato na miongoni mwa fedha zinazokusanywa zinapelekwa kutekeleza miradi mingine ya kimkakati kama huu wa maegesho kwa lengo la kusisimua  makusanyo ya mapato ya ndani”.


Aidha, Mkurugenzi Mtendaji Magesa amesema katika utanuzi huo kutakuwepo mradi wa ujenzi wa Mgahawa wa chakula (Reustaurant), pamoja na  nyumba za kupumzika madereva na wasaidizi wao  (Rest house).


Katika hatua nyingine, Magesa alieleza namna Halmashauri hiyo inavyoendelea  kunufaika na miradi ya kimkakati iliyojengwa katika Halmashauri hiyo, ikiwemo ule wa kituo cha Kikuu cha mabasi  Mpemba.

Philemon Magesa, Mkurugenzi Halmashauri ya Tunduma. 

Amesema kituo hicho kilichojengwa kwa zaidi  shilingi bilioni 1.6  fedha kutoka serikali kuu kimesaidia kuongeza wigo wa makusanyo ya ndani.


Amesema awali kabla ya kujengwa kwa kituo hicho Kikuu cha mabasi yaendayo mikoani, Halmashauri hiyo ilikuwa ikipata kiasi cha shilingi milioni 150, lakini baada ya ujenzi kukamilika sasa Halmashauri hiyo inakusanya jumla ya shilingi milioni 260 kwa mwaka.


Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE