DC MBOZI AKABIDHI PIPA TAKA VWAWA NA MLOWO TOKA TANROADS
Mkuu wa Wilaya ya Mbozi Ester Mahawe amekabidhi mapipa taka katika miji ya Mlowo na Vwawa yaliotolewa na Wakala wa barabara Tanzania ( Tanroads) kupitia Vikundi vya vinavyofanya wa barabara kuu ya Tanzam.
Ugawaji huo umefanyika siku ya jana kwa kuanza na mji wa Mlowo stendi ya Zamani ambapo Mkuu wa Wilaya akiwa ameongozana na kamati ya usalama ya Wilaya na Viongozi toka Tanroads wakiongozwa na kaimu Meneja Injinia Suleiman Bishanga walikabidhi vifaa hivyo ambavyo vitawekwa kenye maeneo mbalimbali mji wa Mlowo
Diwani wa kata ya Mlowo Jaksoni Mwanda amewashukuru Tanroads kupitia vikundi kwa kuwapatia mapipa hayo kwani wao kama mamlaka ya mji wapo katika mipango ya kuuweka mji huo safi na Vifaa hivyo kwao wanaona ni kama neema iliokuja wakati mwafaka.
( Mkuu wa Wilaya Mbozi akiwa katika picha ya pamojo na vikundi vya usafi)
Wakiwa katika stendi ya mji wa Vwawa ambapo ugawaji huo umefanyika zilipo ofisi ya kata ya Ichenjezya Bahati Mbugi Diwani wa Ichenjezya akiongea kwa niaba ya madiwani wenzie amesema utoaji wa vifaa hivyo ni maandalizi pia ya ujenzi wa barabara ya njia nne ya Tanzam itakayotekelezwa chini ya Tanroads hivyo ni namna gani Tanroada inawajali Wananchi na kuwaomba wanavwawa kujali usafi kwa kutupa taka na kuvitunza vifaa taka.
Kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Wilaya Kaimu Meneja Tanroads Suleimani Bishanga amesema utaratibu wa kugawa vifaa hivyo ni kutokana na maelekezo ya Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa Tanroads kuhakikisha linatengwa fungu kwa ajili ya Vikundi vya Vijana, Wazee na akina Mama ambao kwa upande wa Songwe Vikundi hivyo hutoa huduma ya usafi katika barabara zilizo chini ya Tanroads hivyo kupitia fedha hivyo wameamua kutengeneza mapipa ya usafi 54 na kuyagawa katika miji ya Mlowo na Vwawa.
( Wananchi mji wa Vwawa wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya)
"Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya Mkoa wa Songwe bado tunachangamoto ya Vijana kujitokeza kama Vikundi na kuweza kupatiwa mikataba ya ufanyaji usafi barabara zetu tuna vikundi vichache sana vilivyojitokeza kufanya kazi nasi" alisema Bishanga
( Afisa tarafa Vwawa Edward Lugongo akifanya utambulisho wa Viongozi wa Mbozi)
Mkuu wa Wilaya Ester Mahawe amemshukuru Rais kwa wazo lake hilo la kutoa mafungu kwa vijana na kuwataka vijana kuchangamkia fursa hiyo iliopo mbele yao kwa kuunda vikundi na kujisajiri ili waweze kupata ajira mkataba hiyo toka Tanroads na kuepukana na ukaaji wa mitaani na kufanya vitendo visivyofaa kwa jamii wakati pesa zipo Tanroads
"Kama ambavyoTanroads wamesema hapa kuna uhaba wa Vikundi vya vijana lakini hapa nawaona Wazee wao tayari wanakikundi chao na wanafanya kazi Tanroads hivi vijana hamuoni aibu kukaa tu bila kazi na kulalamika kuwa ajira hakuna wakati mamilioni yapo Tanroads hebu tubadilike undeni vikundi mkavisajili pale Bomani mfuate taratibu za maombi Tanroads muanze kuchapa kazi" amesema Mahawe
( Kutoka kushoto, Diwani Ichenjezya, Meneja Tanroads na Mkurugenzi Mbozi)
Aidhs mkuu huyo wa Wilaya ametoa wito wa kutupa taka katika mapipa hayo kulipo kutupa ovyo kwa sababu watu wa usafi wapo na wanalipwa na Tanroads.
Nae mwenyekiti wa umoja wa vikundi hivyo Neema Mwaikuju amewashuru Tanroads wa kuwapatia ajira hiyo na kuwafanya bize wakati wote lakini pia amewaomba Wananchi kuzingatia usafi na wao hawatasita kuwachukulia hatua watakao tupa taka kwa makusudi sehemu isiohusika kwa kuwapeleka katika vyombo vya sheria
Nae Mzee Asone Nzowa ambae pia ni katibu wa Vikundi amesema wao kama wazee wamenufaika na mradi huo kama kikundi chao hivyo wanaishukuru serikali ya Mama Samia na wapo nae bega kwa bega.
Comments