POLISI SONGWE YAWASAKA WALIOFANYA MAUAJI MBOZI


 Watu wawili wamekutwa wameuawa katika matukio mawili tofauti katika vijiji vya Bara na Igamba wilayani Mbozi, Mkoa wa Songwe.


Wakati mmoja akikutwa amekutwa amechinjwa, mwingine amekatwa kichani na kitu kinachosadikiwa kuwa na ncha kali.


Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani, hapa Rashid Ngonyani amesema leo Jumanne Julai 25 mwaka huu kuwa Jeshi la polisi mkoani hapa, linawasaka watuhumiwa wa makosa mawili tofauti ya mauaji, ambayo yametokea hapa mkoani Songwe.



Ameelezea tukio la kwanza kuwa lilitokea Julai 22, 2023 saa 21:00 usiku katika kijiji cha Twinzi wilayani hapa, Mwanamke mmoja Hilda Mwambughi (73), mkazi wa kijiji hicho alikutwa ameuawa nyumbani kwake kwa kukatwa kichwani na kitu chenye ncha kali, na watu wasiofahamika ambao waliomvamia nyumbani kwake na kutekeleza tukio hilo.


"Chanzo cha tukio hio hakijafahamika na uchunguzi wa tukio hilo bado unaendelea, na kwamba jeshi la polisi mkoani Songwe linaendelea kuwasaka watuhumiwa wa tukio hilo la mauaji," amesema Ngonyani.


Ngonyani ameelezea tukio lingine la mauaji limetokea Julai 24, 2023 saa 06:49 alfajiri katika kijiji cha Igamba, Kata ya Igamba, wilayani Mbozi; mkoani hapa, ambapo mkazi wa kijiji hicho Festone Mgalah (27), alikutwa ameuawa kwa kuchinjwa shingoni na kitu chenye ncha kali na watu wasiofahamika.


"Katika tukio hili pia tunaoendelea kuwasaka wahusika wa mauaji hayo huku chanzo cha tukio hilo bado akijafahamika mara moja," amesema Kamanda Ngonyani.


Aidha Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe linakemea vikali uwepo wa matukio ya mauaji pia linawataka raia kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo ili kubaini wahalifu walioshiriki katika matukio hayo.

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE