RC SONGWE AKOSHWA NA BARABARA ILOLO-NDOLEZI ASEMA UTALETA MABADILIKO MAKUBWA
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Dr Francis Michael amesema utekelezaji wa mradi wa Babaraba ya lami ya Ilolo - Ndolezi km 11.01 utaleta mabadiliko makubwa kwa wananchi na hasa wakulima kufikisha mazao yao kwa wakati Sokoni.
Akizungumza mara baada ya kufanya ukaguzi wa barabara hiyo akiwa ameongozana na Katibu Tawala Mkoa Happynes Seneda, Mkuu wa wilaya ya Mbozi Esther Mahawe na wataalamu ngazi ya mkoa na maofisa wa Tarura mkoa na wilaya, amedokeza kuwa barabara hiyo itafungua fursa zingine kwa jamii ya kando kando na kata jirani za Iyula, Idiwili, Mlangali na hata Mahenje
Katika taarifa yake meneja Tarura wilaya Mbozi Felix Ngomano, mradi huo utagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 6 milion mia nne na kwamba mradi huo unatarajiwa kutekelezwa kwa m kipindi cha mwaka mmoja na kwamba kwa mwendo wa mkandarasi, mradi huo utakamilika kwa wakati.
Amedokeza kuwa mradi ulipaswa kuanza mwezi April 2023 baada ya uzinduzi wake, hata hivyo kwakuwa mkandarasi aliagiza mitambo na magari mapya nje hivyo taratibu za bandarini zilichelewesha kuanza utekelezaji na kwamba kwakuwa ameshakamilisha kazi itaenda kwa kasi
Comments