UVCCM WATAKIWA KUUNDA JESHI LA KUPAMBANA NA WANAOKASHFU VIONGOZI MITANDAONI

 Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM ) wilaya ya Sengerema wametakiwa kuunda jeshi la kupambana na watu wanaowakashifu viongozi wa Serikali mtandaoni kinyume na utaratibu wa nchi.



Kauli hiyo imetolewa leo Alhamis Julai 20/2023 mwaka huu na Mbunge wa Buchosa Eric Shigongo kwenye Kongamano ya UVCCM linalojadili mambo mbalimbali iliwemo kujikinga na madawala ya kulevya, maambukizi ya ukimwi na ukimwi sambamba na maadili ya vijana kwa viongozi wa umma.


Shigongo amesema kumetokea kundi la watu wanaotukana viongozi mtandaoni juu ya uwekezaji wa Bandari wanashindwa kutoa maoni yao katika njia sahihi badala yake wanatumia njia ya mitandao kuwashambulia viongozi.


“Jambo hili halikubaliki njia pekee ni vijana kuunda jeshi la kupambana na watu hao mtandaoni wajibiwe kwa hoja, amesema Shigongo.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Sengerema Patric Mundeba amesema vijana wako tayari kuhakikisha nchi inakuwasalama kwa kujibu hoja za wapotoshaji ambao hawaitakii mema nchi yetu .


Huku katibu wa UVCCM Wilaya ya Sengerema Adamu Itambu akiwata vijana kuwa wamoja na kuwa wazalendo ndani ya nchi Kwa kukemea maovu na upotishaji unaenezwa na baadhi ya watu wasioitakia mema nchi yetu.


Mmoja wa washiriki katika Kongamano hilo Clara Benedict amesema wamepokea maelekezo ya viongozi wao wako tayari kiyatekeleza.


UVCCM wametakiwa kuwa wamoja na kuisemea serikali juu ya mambo yanayofanywa na Serikali ya kuwaletea wananchi maendeleo.

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE