DC ILEJE AWATAKA WAMAMA KUTENGA MUDA KUWANYONYESHA WATOTO
MKUU wa wilaya ya Ileje mkoani Songwe Mhe.Farida Mgomi ametoa rai kwa jamii wakiwemo waajiri na kinababa Mkoani humo kutoa ushirikiano wa kutosha kwa kinamama wanaonyonyesha watoto ili waweze kuwanyonyesha watoto wao katika hali ya utulivu ikiwemo kuweka mazingira wezeshi ili unyonyeshaji huo ufanyike kwa tija kwa watoto.
Mhe. Mgomi ametoa rai hiyo Agosti 7,2023 wakati akiwasilisha hotuba katika kilele Cha wiki ya unyonyeshaji kimkoa akimwakilisha mgeni rasmi ambaye alikuwa mkuu wa mkoa wa Songwe Dkt. Francis Michael ambayo kimkoa imefanyika katika kijiji Cha Msia kata ya Chitete wilayani Ileje.
Mhe. Mgomi amesema ili unyonyeshaji ukamilike lazima kuwe na usaidizi upande mwingine ,ambapo pia mama anajukumu la kunyinyesha Kila siku nakupanga majukumu yake vizuri.
"Kuna kila sababu wababa(waume) kusaidia unyonyeshaji kwani suala la unyonyeshaji sio la baba na mama bali jamii kwa ujumla kwani mtoto anatakiwa kupata maziwa ya mama tangu anapozaliwa mpaka miaka 2," amesema Mhe.Mgomi.
Mhe.Mgomi amesema wanawake wanapaswa kutumia matiti kunyonyesha kinyume chake itapelekea mtoto kuathiririka kiafya ikiwepo udumavu Kwa kukosa baadhi ya madini yanayopatikana kwenye maziwa ya mama.
Mhe Mgomi amesema mkoa wa Songwe una udumavu Kwa asilimia 31.9 ,na kitaifa mkoa una asilimia 30.
Aidha Mhe.Mgomi amesema mtoto akifanikiwa kunyonya maziwa ya mama ake Kwa siku 1000 anakuwa na afya njema ,hivyo nawasihi wababa kuwalewa watoto Kwa kuwatengea muda mzuri wa kunyonya ili apate virutubisho vyote vya chakula kupitia maziwa ya mama.
"Niwatahadhilisheni wazazi wenzangu hakikisheni zingatieni ushauri wa wataalamu kuwanyonyesha maziwa ya kwanza ya mama ,na kutokumpa chakula kingine kwa miezi 6 ,msiwalishe viazi,mihogo, Ndizi kabla ya miezi hiyo utakuwa unamtengenezea udumavu katika makuzi yake ambapo baada ya miezi 6 umpatie chakula Kwa kuzingatia makundi ya chakula", amesema Mhe.Mgomi.
Aidha Mhe. Mgomi akizungumza katika sehemu ya wasilisho lake amesema Baba anapaswa kuwajibika kwa kuweka mazingira wezeshi ili kumfanya Mama aweze kunyonyesha Mtoto wake kwa utulivu bila ya kuathiri hali hiyo ya unyonyeshaji.
Ikumbukwe wiki hii ya unyonyeshaji ya Mama huadhimishwa kila mwaka ifikapo tarehe 1 mwezi wa nane ya kila mwaka na kilele chake huhitimishwa tarehe 7 ya mwezi huu ambapo kaulimbiu ya mwaka huu inasema, " SAIDIA UNYONYESHAJI WEZESHA WAZAZI KULEA WATOTO NA KUFANYA KAZI ZA KILA SIKU.

Maoni