DC ILEJE AWATAKA WANANCHI KUTUNZA MIUNDOMBINU NA KUOMBA UMEME

Mkuu wa wilaya ya Ileje mkoani Songwe  Mhe. Farida Mgomi amewataka wananchi wa Wilaya hiyo kutunza na kulinda miundombinu ya umeme huku akiwataka kuhakikisha wanatumia umeme kwa usalama.


Mhe. Mgomi ametoa rai hiyo Agosti 4, 2023  wakati mwenyekiti wa bodi ya wakala wa nishati vijijini REA Janeth Mbene katika vijiji vya Ibandi kata ya Kalembo na Kijiji cha Shinji Kata ya Mbebe akizindua mradi wa nishati mzunguko wa pili katika kata hizo.

Mhe. Mgomi amesema kama umeme umefika kwenye vijiji vyao mnatakiwa kubaini fursa zinazoweza kuwaingizia kipato kwenye maisha ya kila siku.


"Tumeona serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dk.Samia Suluhu Hassan  imetoa fedha nyingi sana itashangazwa tuanfurahia tu kuwaka kwa taa ,badala ya kujitengenezea miradi itakayotumia nishati hiyo", amesema.Mhe. Mgomi.


Mhe.Mgomi amezitaka halmashauri za vijiji kuhakikisha tunatunza miundombinu ya umeme ikiwepo kudhibiti kuchoma moto na kuharibu nguzo ni marufuku.

"Ni marufuku kuona nguzo zinaharibika kwa kuchoma moto ,nikiliona hili  linatokea sitakubaliana nalo kwani serikali imetoa fedha nyingi kwa kuwanufaisha wananchi alafu nyinyi mchome miundombinu ", amesema Mhe.Mgomi.


Amesema "Rai yangu mtunze na kulinda miundombinu hii na mhakikishe kuwa matumizi ya umeme yanatumika salama hasa kwa vijana wadogo ameendelea kusema Mhe.Mgomi

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Umeme Vijijini, Janeth Mbene amesema kuwa Serikali imeweka historia kupeleka umeme vijijini ikiwemo katika vijiji vya Ibandi na Shinji  Wilayani Ileje ambayo ilikuwa haijapata umeme tangu uhuru.


"Kwa bahati nzuri fedha za kuendesha nishati vijijini zipo mama yetu (Rais Samia) anahakikisha kuwa hela haikomi kutokana na vyanzo mbalimbali ambavyo vipo serikalini Lengo la kuleta umeme ni kuchochea uchumi" amesema Mbene.




Kwa upande wake  Mkurugenzi Mtendaji wa REA Mhandisi Hassan Said amewatahadharisha wananchi kutokufanya shughuli za kijamii chini ya laini kubwa ya kupitisha umeme.


Pia Mhandisi Said amewahakikishia wananchi wa Ileje kuwa serikali imetoa hela za kutosha kuhakikisha miradi hii sasa inafika katika ngazi za vitongoji na wilaya ya Ileje itafikiwa na Vitongoji zaidi ya mia moja (100).


Meneja wa TANESCO  Kanda nyanda za juu Kusini Magharibi Mhamdisi Sotko Nombo amewataka wananchi wa kata hiyo kuomba kuunganishiwa umeme ambapo gharama yake ni Sh.27, 000 kwa maeneo hayo ya vijijini pamoja na kununua kifaa Cha UMETA ambacho kinarahisisha kuingiza umeme pindi unapokuwa hunagharama za kusuka waya kwenye  nyumba zenu.


"Niwambieni ndugu zangu hata kama utashindwa kusuka waaya kwa ajili ya kuweka umeme kwenye nyumba zenu nunueni  kifaa kinaitwa  UMETA kwa gharama ya shilingi 50,000 ili upate umeme kwa matumizi ya majumbani", amesema Mhandisi Nombo,".

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

KUMBUKUMBU YA MAISHA YA MH. ESTER ALEXANDER MAHAWE

CONSTRUCTION OF THE ISONGOLE-ISOKO ASPHALT ROAD IS NOW OFFICIAL, CONTRACTOR INTRODUCED TO THE PUBLIC

*KUNDO AGOMA KUWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA MAJI VWAWA-MLOWO