KAMANDA WA POLISI SONGWE APELEKA SOMO LA UKATILI WA KIJINSIA KANISANI TUNDUMA ATOA WITO
Kamanda wa polisi mkoa wa songwe kamishna msaidizi wa jeshi la polisi Theopista Mallya ametembelea kanisa la Ufufuo na Uzima lililopo chini ya mchungaji Edwine Sostenes katika mtaa wa Nyerere mjini Tunduma wilaya ya Momba mkoani Songwe
Kamanda wa polisi mkoa wa songwe alipata nafasi ya kutoa elimu kwa waumini wa kanisa hilo
Katika mambo mbalimbali ambayo yanapelekea matendo maovyo na kupelekea ukatili wa kijinsia na uhalifu, Ikiwa pamoja na Rushwa,Ulawiti,Tamaa ya mali,Kubaka,Wivu wa Mapenzi,Ushoga Migogoro ya ardhi, Ulevi uliokithili,Imani za kishirikina, Huduma za polisi ni bure,Kudhini na ndugu wa damu na pia Wananchi kushirikiana na jeshi la polisi kwa kutoa taarifa za wahalifu na uhalifu ili kutokomeza vitendo hivyo katika maeneo yao yanayowazunguka.
Aidha elimu hiyo imetolewa kwa kutumia vifungu mbalimbali vya maandiko katika Biblia vinavyozungumzia mambo hayo, Sambamba na hayo aliyataja madhara ya vitendo hivyo ikiwa pamoja na Matatizo ya akili, ulemavu, kujitenga na marafiki au familia, kifo na kufungwa jela.
Kamanda wa polisi mkoa wa songwe amewahasa vijana kuwatii wazazi wao na kufanyakazi kwa bidii, hii itawaepusha kutokujiingiza kwenye matendo maovu ambavyo vitawapelekea kufanya uhalifu na vitendo vya kiuhalifu, aliongezea kwa kusema wanafunzi wanatakiwa kuzingatia masomo yao na kuacha kujihusisha na mahusiano ya kimapenzi ili kuweza kutimiza malengo yao katika masomo yao na maisha yao kwani vijana ni taifa la leo.
Leo agosti 20, 2023 majira ya saa 10:30hrs hadi 14:00hrs Kamanda wa polisi mkoa wa songwe kamishna msaidizi wa jeshi la polisi Theopista Mallya ametembelea kanisa la Ufufuo na Uzima lililopo chini ya mchungaji Edwine Sostenes katika mtaa wa Nyerere mjini Tunduma wilaya ya Momba mkoani Songwe

Maoni