PAPII KOCHA AONDOKA TUKUYU SOUND NA KUJIUNGA TOWN CLASSIC
Msanii wa Muziki wa Dansi Papii Kocha almaarufu kama mtoto ametua rasmi katika bendi ya Town Classic.
Kwa mujibu wake Papii amesema kuwa ameamua kuondoka Tukuyu si kwa ubaya na tayari amewajulisha walezi wa bendi hiyo Alnanuswe Kabungo na Benjamini Mwandete pia amewaaga wanamuzi wenzie ikiwemo Mkurugenzi mwenzie Kalala Junior
"Mimi nimeondoka kwa wema ndio maana niwaaga wote kwa wema kuanzia walezi wangu mpaka wanamuzi wenzangu"-Papii
Aidha Papii amewataka mashabiki wa Tukuyu kutomuona yeye ni adui kisa tu yeye kusaini mkataba na Town Classic ni kwamba ameamua kwenda kujifunza changamoto mpya za kimaisha.
Nae mmoja wa walezi wa bendi ya Tukuyu sound Benjamin Mwandete amethibitisha kuondoka kwa Papii Kocha na wenzie watatu na amesema ni kweli wameondoka kwa kuaga na wamewapa baraka zote
"Mwandishi haya ni maisha na wao wanatafuta maisha kama huko walikokwenda wameona kuna maslahi hakuna wa kupinga Papii ni mtoto wetu kaaga vizuri nyumbani na tumemwambia akiona hakueleweki basi arudi nyumbani kubwa hajachafua barazani kwetu" Mwandete

Maoni