RAIS SAMIA ATENGUA UTEUZI WA KATIBU WA WIZARA YA MAJI


 Rais Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Katibu Mkuu Wizara ya Maji Nadhifa Kemikimba.


Kemikimba aliteuliwa kushika nafasi hiyo  Februari 26, 2023 na aliapishwa kushika wadhifa huo katika hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma Februari 27, 2023.


Awali alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo na amewahi pia kutumikia nafasi mbalimbali ikiwamo Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Ubora wa Maji.


Taarifa ya kutenguliwa kwake imetolewa leo Ijumaa Agosti 18, 2023 na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu Zuhura Yunus

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

UDUMAVU BADO TISHIO -DUGANGE

SONGWE JOGGING WARUDI NA MEDANI ZAIDI YA KUMI NA TANO TULIA MARATHON

MOMBA HAWANA JAMBO DOGO: ROUTE VIONGOZI NA WANANCHI WAKUTANA PAMOJA ROUTER MATCH YANOGA