TASISISi ZA SERIKALI ZATAKIWA KUBORESHA HUDUMA KUVUTIA SEKTA BINAFSI




Songwe. Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe amezitaka taasisi za Serikali kuboresha huduma ili kuwezesha sekta binafsi kufanya biashara mipakani kwa uhuru.


Naibu waziri huyo ameyasema hayo leo Jumatano Agosti 9, 2023 wakati wa ziara yake ya siku mbili mkoani Songwe.

"Nipo hapa kwaajili ya mpango wa kuboresha mazingira ya sekta binafsi ambayo ni maelekezo ya Rais Samia kuboresha sekta binafsi ambayo ni injini ya uchumi wa Tanzania na Dunia kwa ujumla" amesema  na kuongeza;


"Ujue wa sekta binafsi ikisimamiwa vizuri inafanya vizuri.Tunataka kuona taasisi za Serikali zinawezesha taasisi binafsi kupata huduma bila vikwazo ili kurahisisha ufanyikaji wa biashara katika mpaka wa Tunduma" 


Kigahe amewaagiza wakala wa vipimo kukagua bidhaa ili kupata thamani ya kilichofungashwa.


"Mkuu wa mkoa wa Songwe ametupa ushirikiano ambapo tunaona wakulima watapata stahiki zao kwa kupima uzito ulio sahihi kwa mizani tofauti na sasa wanavyotumia BP, ndoo na lumbesa" amesema na kuongeza

Kwa kufanya hivyo itawafanya hata halmashauri kupata mapato halisi kwa kuwa na ujazo halisi wa bidhaa" ameeleza naibu waziri huyo


Amewataka Wakala wa Vipimo watoe elimu kwa wakulima ili wazalishe zaidi na kuona faida ya kulima.



"TBS hakikisheni bidhaa inayoingia iwe na viwango tulivyo kubaliana na ubora unaotakiwa. Tuwe makini na watu wanaofanya lebo katika bidhaa kama wakatumia mwanya bidhaa ikipelekwa kwa mkemia huku wakibaki wanasambaza bidhaa feki tuone namna ya kuboresha vibali" ameagiza


"Tuone ambayo tunapunguza vikwazo vya biashara nchi za Afrika tofauti na sasa tusiwekeane vikwazo kwa kuchaji tozo kubwa. Tusaidieni wataalamu tuboreshe uingizwaji wa bidhaa bila kuathiri makubaliano yetu" 

"Na sisi Tanzania tuwe wa kwanza kuviondoa vikwazo naamini tumejipanga vizuri" amebainisha naibu waziri huyo na kuongeza


Nimefurahi sekta zote uhamiaji, Usalama, TRA, wakala wa vipimo, TBS tunavyoboresha huduma nchi nyingi zitapita kwetu, ninyi ndio kioo chetu na kupitia ninyi kutoa huduma nzuri tutaiweka nchi katika taswira nzuri ya kibiashara"


Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Dk Francis Michael amesema kuwa Songwe ni mkoa wa kimkakati na wamejipanga kuwaita wawekezaji kuwekeza zaidi katika sekta ya viwanda vitakavyozalisha mchele kutokana na mkoa huo kuzalisha mchele bora na usiotumia mbolea.


Dk Michael amesema wawekezaji wakija kama mkoa zao la mpunga litaongezewa thamani na wakulima watanufaika.


Mkuu wa mkoa huyo amewataka Sido kujenga ofisi yao karibu na ofisi za makao makuu ya mkoa wa Songwe ili kurahisisha wananchi kupata huduma jirani.


Meneja wa Wakala wa Vipimo wa Mkoa wa Songwe, Siraji Moyo amesema kuwa bado wanaendelea kutoa elimu na kufanya kaguzi kwa wafanyabiashara wanaotumia lumbesa na BP ili kuweza kuondokana na mfumo huo.


Naibu waziri huyo ametembelea eneo lililotengwa kwaajili ya viwanda vidogo la Sido Kijiji cha Zelezeta wilayani Mbozi, Ofisi za Wakala wa Vipimo Mkoa wa Songwe na Kituo cha pamoja cha Tunduma katika mpaka wa Tanzania na Zambia

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

UDUMAVU BADO TISHIO -DUGANGE

SONGWE JOGGING WARUDI NA MEDANI ZAIDI YA KUMI NA TANO TULIA MARATHON

MOMBA HAWANA JAMBO DOGO: ROUTE VIONGOZI NA WANANCHI WAKUTANA PAMOJA ROUTER MATCH YANOGA