DC ILEJE, TANROADS WAFANYA KIKAO,WANANCHI KUANZA KULIPWA FIDIA
Mkuu wa Wilaya ya Ileje Farida Magomi ameongoza kikao kazi pamoja na Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) chenye lengo la kuunda Kamati ya Usuluhishi wa malalamiko yatokanayo na fidia kwa ajili ya ujenzi wa Barabara ndani ya Wilaya ya Ileje kutoka Isongole-Isoko kwa awamu ya kwanza yenye urefu urefu wa Kilomita 52.414 kwa thamani ya Shilingi za Kitanzania 850,265,900.70
( Wajumbe wa kikao wakiwa ofisini kwa Dc Ileje Itumba)Kikao hicho kimefanyika leo Septemba 18,2023 kwenye Ofisi za Mkuu wa Wilaya zilizopo Itumba-Ileje.
Sambamba na uundwaji wa Kamati hiyo, Wakala ya Barabara nchini Tanzania (TANROADS) unatarajia kuanza kutekeleza malipo kwa wahusika mnamo Septemba 19,2023.
(Nuru Kindamba Mkurugenzi Halmashauri ya Ileje)
Comments