MBOZI WAZINDUA KAMPENI YA KUGAWA TAULO ZA KIKE SHULE ZOTE,DC ATAKA ZIRO ZITOKOMEZWE

Mkuu wa Wilaya ya Mbozi Esther Mahawe ametoa wito kwa walimu na wanafunzi ndani ya Wilaya ya Mbozi kuhakikisha wanatokomeza division zero katika mtihani wa kidato cha nne.


Ametoa wito huo leo Jumanne Septemba 19, 2023 wakati wa hafla ya ugawaji wa taulo za kike kwa wanafunzi wa kike katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi.

 Ester Mahawe Mkuu wa Wilaya ya Mbozi

Amesema kuwa taulo hizo zenye thamani ya Sh15 milioni za mapato ya ndani, zitagawiwa kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari za Serikali ambapo jumla ni wanafunzi 34827.


"Kusema ukweli kazi inafanyika katika awamu ya sita chini ya kiongozi wetu Mama Samia Suluhu Hassan. Sasa hivi mnasoma katika mazingira rafiki sana madarasa yana tiles ya vioo vyoo vizuri huwezi kulinganisha kabisa na sisi tulikotoka" amesema 

            ( Waalimu wa shule mbalimbali              wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya)


"Sasa ninyi leo sijui mtakuwa na excuse gani mnasoma katika mazingira mazuri.

Lakini zamani mwanafunzi wakike katika siku zile 194 anazotakiwa kuwepo shuleni karibu siku 50 alikuwa anashindwa kufika shuleni akiingia katika ule mzunguko anashindwa kuja shuleni kwasababu mazingira hayajakaa vizuri" ameeleza


Amesema kuwa kwa sasa mazingira ni mazuri  hivyo wajitahidi katika masomo kuonyesha shukrani kwa Rais Samia.


"Naomba niwasisitize wenzangu katika Wilaya ya Mbozi tuhakikishe tunatokomeza divisheni ziro na four. Inawezekana sana, penye nia pana njia"


Amesema yeye ni miongoni mwa Wabunge wakike waliokuwa wanasisitiza suala la taulo za kike zigawiwe bure 

    Aidha amesema kipindi nyuma zamani walikuwepo Watoto wa kike ambao walikuwa wanashindwa kuhudhulia masomo kutokana kukosa taulo  za kike kutokana na changamoto za kipato za wazazi wao lakini serikali ya awamu ya sita chini yake Rais Dtk Samia imeamua kugawa taulo za kike bure hivyo wanafunzi hawana sababu ya kuwa na matokeo mabaya ya darasa sababu wanapata muda mzuri wa kuhudhulia masomo yako.

Pia Dc amewataka waalimu wao wanafunzi kuhakikisha wanazidisha juhudi za kufundisha ili watoto hao wa kike waweze kuwa na ufaulu Mzuri na hiyo ndio itakuwa zawadi na bora kwa Mhe Rais.

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE