WAKULIMA WAHAMASISHWA KUTUMIA MBOLEA MOMBA
Wakulima halmashauri ya Momba tarafa ya Msangano na Kamsamba wametakiwa kuondokana na dhana potofu ya kwamba kutumia mbolea kunaharibu mazao kwani kwa kufanya hivyo ni kujichelewesha wenyewe kupata mafanikio.
Hayo yamesemwa na mtaalamu wa masula ya mbolea kutoka shirikisho la vyama vya ushirika TFC Carlos Ndumbarobwakati wa semina zinazoendelea kwa wakulima halmashauri ya Momba na timu ya wataalamu kutoka wizara ya kilimo na ushirika waliokita kambi ya siku 14 kutoa elimu ya kilimo bora na chenye tija kwa kwa wakuliama.
“Haya mawazo tunaomba wakulima wa huku bondeni muachene nayo kabisa kwani yanawachelewesha kufikia mafanikio, kwa karne hii huwezi kukwepa matumizi ya mbolea, kwanza ardhi imechoka inahitaji kuiongezea rutuba kupitia mbole” Ndumbaro
Kwaupande wake mratibu wa utafiti na ubinifu kutoka taasisi ya utafiti wa kilimo Tanzania Tari-Ilonga Meshack Makenge, amesema mafanikio mengine katika kilimo ni wakulima kuzingatia uchagzi sahihi wa mbegu na kupanda kwa utaalam.
“Tunapozungumzia kilimo biashara na chenye kuleta tija matumizi ya mbegu bora ni jambo la msingi sana, matumizi ya mbegu za asili zinakufanya wewe mkulima kutumia nguvu kubwa kwa kulima shamba kubwa laikini mavuno kidogo” Makenge.
Mratibu wa uhaulisha wa teknolojia na mahusiano Tari-Ilonga, Lilian Mwanga amesema katika kuwasaidia wa kulima taasisi ya utafiti wa kilimo Tanzania inazo teknolojia mbalimbali za kisasa zinazomwezesha mkulima kufikia mafanikio ya haraka kupitia sekta ya kilimo.
“Tunapozungumzia teknolojia ni pamoja na mbegu bora za mazao mbalimbali, ikiwemo mahindi, alizeti, mtama, ufuta na mazoa yote ya mikunde ambayo, kwa asilimia kubwa tasisi yetu ya Tari inazalisha” Mwanga
Rosemary Simchimba na Daud Mtaturu ni wakulima wa kijiji cha Mkomba, wamesema changamoto inayosababisha wakulima wa Momba ukanda wa chini kutotumia mbolea walikosa elimu ya matumizi sahihi ya mbolea hizo na hata hivyo mbole hizo hazifiki kwa wakati na hata upatikanaji wake ni mgumu.
“Walikuja wataalamu hapa kijijini kwetu wakatuandikisha na kuchukua majina yetu kwa ajili ya mbolea, laki cha kushangaza awamu zote mbili hawakutuletea mbolea na ndiyo maana tulikata tama na kuendelea kulima kama tulivyo zoea miaka yote” Simchimba.
Kwaupande wake Mbunge wa Jimbo la Momba Mheshimiwa Condester Sichalwe, amesema kipindi hiki ambacho yeye ndiye mbunge anatamani kuona watu wake wanakomboka na kilimo cha utumwa kisichokuwa na manufaa.
Comments