DC ILEJE ATANGAZA KIAMA KWA WAVAMIZI WA MSITU KYOSA HEKTA 600


Wananchi vijiji vya Ndapwa kata Ngulilo wilaya ya Ileje mkoa wa Songwe na Kijiji Cha Kiobo wilaya ya Rungwe mkoa wa Mbeya wametakiwa kuondoka na kuacha na uvamizi kwenye hifadhi ya  msitu Kyosa uliopo Kijiji Cha Ndapwa wilayani Ileje Kwa kufuata kanuni na Sheria za misitu.


Agizo hilo limetolewa Oktoba 3,2023 na mkuu wa wilaya ya Ileje Farida Mgomi wakati akizungumza na wananchi wa Kijiji Cha Ndapwa kwenye mkutano wa hadhara kwenye kampeni ya oparesheni ya uhifadhi wa misitu uliondaliwa na ofisi ya wakala wa huduma za misitu Tanzania shamba la miti  Iyondo Mswima wilayani humo (TFS).

Mgomi amesema uvamizi kwenye hifadhi hiyo umefanywa na wananchi kinyume na taribu na kupelekea zaidi ya hekta 600 sawa na asilimia 60 kati ya zaidi ya hekta 1000 hali ambayo inahatarisha kupoteza uoto wetu.


"Kutokana na uharibifu huo nitoe tamko Kwa wananchi wote waliovamia hifadhi ya msitu wa Kihosa waondoke mara Moja licha ya kwamba shughuli zao zinafanywa usiku serikali Iko macho itawashughulikia," amesema Mgomi.


Mgomi amesema baada ya tamko hilo la kuwataka wananchi waliovamia msitu huo na kufanya shughuli za kibinadamu  kuondoka pindi watakapokaidi hatua Kali za kisheria zinachukuliwa bali waendelee kuwa mabalozi wa kutoa elimu kwa wananchi umuhimu wa kuhifadhi mazingira.


Mgomi amesema wataalamu wa misitu wameendelea kutoa elimu na Sasa ofisi ya wakala wa huduma za misitu Tanzania TFS wameandaa kampeni maalumu ya kutoa elimu Kwa jamii juu ya madhara ya moto, uharibifu wa misitu na faida za uhifadhi wa misitu Ili kuhakikisha wananchi wanatambua hasara za ukataji na uchomaji moto misitu.

Katika kuhakikisha utunzaji wa mazingira unakuwa endelevu meneja wa misitu Omary Abeid Aalli amesimamia zoezi la kuchagua wajumbe 10 ambao watakuwa na jukumu la kuhakikisha uvamizi, uharibifu kwenye hifadhi ya misitu Kyosa haujitokezi tena.


Mwenyekiti wa kamati iliyochaguliwa Elius Cheyo amesema watatengeneza ushirikiano na wananchi kuhakikisha wavamizi wanaolima kwenye mashamba yaliyopo kwenye hifadhi wanaondoka na kushirikiana kupanda miti Disemba mwaka huu kama ilivyoahidiwa na TFS.

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE