DEREVA WA DC MBOZI ADONDOKA WAKATI DC AKIENDELEA NA MKUTANO NA WANANCHI AFARIKI DUNIA HOSPITALI
Dereva wa Mkuu wa Wilaya ya Mbozi anaefahamika kwa majina ya Goodluck Mbazu amefariki katika hospital ya rufaa Mkoani Mbeya ambapo alikimbizwa baada ya kudondoka wakati akitaka kushuka kwenye gari alilokuwa amepumzika wakati Mkuu wa Wilaya ya Mbozi Esther Mahawe akieendelea kuwahutubia Wananchi katika Mkutano wa wa utatuzi wa mgogoro Kijiji cha Shaji kata ya Mlangali.
Akiongea kwa njia ya simu Mkuu wa Wilaya ya Mbozi ambae alishindwa kuongea vizuri kutoka na kuwa katika hali ya kushindwa kuamini kifo cha dereva wake huyo amesema alikuwa ni sehemu ya familia yake na aliishie nae kama ndugu hivyo kifo chake cha ghafla kimemuumiza na kushindwa kuamini kwani ndie aliwapeleka katika Mkutano huo Kijiji cha Shaji na alikuwa na afya njema lakini alipomaliza Mkutano aliarifwa kuwa dereva wake amekimbizwa hospitali baada ya kadondoka wakati akishuka katika gari alilukiwa amekaa na dereva mwenzie wakipumzika .
"Nilalifiwa kuwa dereva wangu alianguka wakati akijaribu kushuka kwenye gari alilokuwa kapumzika na dereva mwenzio ambapo dereva wangu alikuwa akioongea na simu na alipopelekwa hospitali presha yake ilikuwa juu na ilipelekea baadhi ya mishipa kupasuka kichwani na kumpeleka umauti,kwakweli hiki kifo cha huyu dereva kimeniumiza sababu siku si nyingi alinipeleka kumuoma Mama yake na akaniambia anataka kumakarabatia Mama yake nyumba yake na ukizingatia Mama yake umri wake umeenda lakini kabla ya kutimiza malengo aliyoyapanga Mwenyezi Mungu kamchukua kubwa tumuombee huko alipo apumzike kwa amani" alisema Mahawe.
Kwa upande wa Wananchi wa Mbozi waliokiwa wakimfahau vyema dereva huyo aliwepo Ibu Mwanjilinji amesema kwao ni pigo kwani Mbazu alikuwa na nidhamu Kubwa ya Kiutumishi na alikuwa akiishi vyema na watu hivyo Wana Mbozi wamepata pigo kubwa.
Kwa upande wa dereva mwenzio Frank Kilasi maarufu kama Tugu amesema wameshtushwa na msiba wa dereva mwenzao na hawana mengi ya kusema zaidi ya kumuombea na sasa wanaendelea na michango ili kuhakikisha wanashiriki vyema katika jukumu la kumstiri Mbazu
Comments